Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Winga Yanga awindwa Coastal Union

Muktasari:

  • Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zimeliambia Mwanaspoti, Farid ni miongoni mwa wachezaji wanaopigiwa hesabu za kujiunga na Coastal Union na mazungumzo yameanza kati ya pande zote mbili, japo hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa hadi sasa.

UONGOZI wa Coastal Union umeanza hesabu za kuiwinda saini ya winga wa Yanga, Farid Mussa ili kuongeza nguvu ya timu hiyo kwa ajili ya msimu wa 2026-2027, baada ya nyota huyo kumaliza mkataba na mabingwa hao wa Ligi Kuu msimu wa 2025-2026.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zimeliambia Mwanaspoti, Farid ni miongoni mwa wachezaji wanaopigiwa hesabu za kujiunga na Coastal Union na mazungumzo yameanza kati ya pande zote mbili, japo hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa hadi sasa.

“Ni kweli Farid yupo katika mipango yetu na ikiwa kila kitu kitaenda sawa basi tunaweza kukamilisha uhamisho huo, suala lililopo kwa sasa ni kufanyia kazi maslahi yake binafsi, jambo ambalo bado tunaendelea nalo,” kilisema chanzo hicho.

Akizungumza na Mwanaspoti, Katibu Mkuu wa Coastal Union, Omary Ayoub alisema mchezaji yeyote watakayefikia makubaliano naye watamtambulisha rasmi katika kurasa zao za mitandano ya kijamii, japo kwa sasa hawezi kuzungumzia suala la Farid.

Mwanaspoti linatambua, Farid mkataba wake na Yanga umeisha na hakuna mazungumzo mapya yanayoendelea, jambo linalofungua milango kwa timu mbalimbali kuiwinda saini yake, huku Coastal Union ikiongoza licha ya kutofikia makubaliano hayo rasmi.

Farid ni miongoni mwa wachezaji wazawa waliocheza soka nje ya Afrika akiitumikia CD Tenerife B ya Hispania akitokea Azam, kisha aliporejea Tanzania ndipo akatua Yanga Agosti 12, 2020.