Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TRA United yawakusanya wataalamu

TRA United

Muktasari:

  • TRA United baada ya mechi sita ilikuwa na ushindi mmoja, sare tatu na vipigo viwili, ikiweka rekodi ya kufunga mabao sita na kufungwa sita ikifikisha jumla ya pointi sita katika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi.

TRA UNITED imeanza kujenga sura mpya ndani ya benchi lake la ufundi kwa kuvuta wataalamu kutoka vigogo wa Yanga na Azam FC, ikiwa hesabu za kuimarisha kikosi hicho msimu huu.

TRA United baada ya mechi sita ilikuwa na ushindi mmoja, sare tatu na vipigo viwili, ikiweka rekodi ya kufunga mabao sita na kufungwa sita ikifikisha jumla ya pointi sita katika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi.

Baada ya klabu hiyo kumchukua mtaalamu aliyekuwa akifanya kazi Yanga, sasa imeongeza nguvu nyingine kwa kumsajili Murshid Kika, aliyekuwa kocha wa mazoezi ya viungo wa Azam FC, akiwa na jukumu la kusimamia utimamu wa mwili wa wachezaji.

Taarifa za ndani zililiambia Mwanaspoti; “Tumekuwa tukisajili kutokana na mahitaji yetu na kuzingatia ubora wa wachezaji pamoja na nafasi ambazo tulihitaji kuzifanyia maboresho, ndio maana tunaendelea kuongeza nguvu hasa kwenye eneo la ufundi ili mastaa wazidi kunolewa.”

Ujio wa Murshid unaifanya TRA United kuwa na mtu aliyepitia mazingira ya Azam, moja ya timu zinazoshindana kileleni mwa ligi, huku klabu hiyo ikiwa tayari imekuwa ikivuna wataalamu wenye uzoefu kutoka Yanga.

Hatua hiyo inakuja wakati ambao TRA United inahitaji kuongeza ubora katika kila eneo, hasa baada ya kuanza msimu wa 2026/27 ikiwa bado inatafuta muunganiko mzuri wa kikosi kipya. Wakati huo huo TRA United imeanza mazungumzo ya dhati kumsajili mtaalamu wa uchambuzi wa mbinu na utendaji wa wachezaji (Performance & Tactical Analyst) wa Yanga, Bartalomew Prosper

Mchakato huo unatokana na mapendekezo ya Kocha Mkuu mpya wa TRA United, Hemed Suleiman ‘Morocco’, ambaye anataka kuongeza nguvu na kuimarisha ufanisi wa benchi lake la ufundi klabuni hapo.