Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Winga Mlandege afichua jambo

Muktasari:

  • Nickson alisema timu bado haijawa katika mpangilio mzuri kwa wachezaji, ingawa wanaendelea kutuliza presha ya ligi kwa lengo la kutafuta matokeo mazuri kwenye mzunguko wa kwanza.

WINGA wa Mlandege, Boniphace Nickson amesema hayakuwa malengo ya timu kuanza msimu vibaya lakini imetokea, hivyo wanajipanga kuhakikisha timu inakaa sawa.

Nickson alisema timu bado haijawa katika mpangilio mzuri kwa wachezaji, ingawa wanaendelea kutuliza presha ya ligi kwa lengo la kutafuta matokeo mazuri kwenye mzunguko wa kwanza.

Alisema Baadhi ya wachezaji wa timu hiyo hawana uzoefu wa kucheza Ligi Kuu ndio kwa maana hiyo wanakuwa na hofu wakicheza, hali hiyo imekuwa ikiitesa timu.

"Siyo malengo yetu kuanza ligi vibaya naamini muda si mrefu tutarudi kwenye ubora wetu ambao umezoeleka, baadhi ya wachezaji wana hofu," alisema Nickson.

Alieleza kuwa makocha wa timu hiyo wanaendelea kuwatuliza wachezaji kisaikolojia kwani ligi inaendelea kuwa na ushindani, huku akisisitiza kwamba endapo wachezaji hawatakuwa makini wakiendelea na mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha kuna balaa kubwa katika mechi zijazo.

Mchezaji huyo aliwaomba mashabiki wao wasichoke kuwaunga mkono katika kipindi hiki kwa sababu wanaamini watakaa sawa na kuwapa furaha.

Mlandege ipo nafasi 10 ya msimamo wa ligi hiyo ina pointi nane kati ya michezo saba iliyocheza, imeshinda miwili na kupoteza  mitatu huku ikitoa sare miwili.