Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kigogo DRFA afariki dunia, TFF, wadau waomboleza

Muktasari:

  • Kanuti ameutumikia mpira wa miguu kwa zaidi ya miaka 30 akihudumu katika nafasi tofauti kwa ngazi ya mkoa na wilaya ya Ilala.

Vyama vya Mpira wa Miguu Dar es Salam (DRFA) na Ilala (IDFA) vimepata pigo kufuatia kifo cha ghafla cha mtumishi na kiongozi wa vyama hivyo, Daud Kanuni usiku wa kuamkia leo, Oktoba 17, 2026.

Taarifa za awali zinaripoti kwamba Marehemu Kanuti alibanwa ghafla na kifua, tatizo ambalo limekuwa sababu ya kifo chake.

Kanuti ameutumikia mpira wa miguu kwa zaidi ya miaka 30 akihudumu katika nafasi tofauti kwa ngazi ya mkoa na wilaya ya Ilala.

Wadau mbalimbali wameonyesha kuguswa na kifo cha Kanuti ambaye hadi anafariki, alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ilala (IDFA).

"Marehemu Kanuti atakumbukwa kwa mchango wake katika utumishi na maendeleo ya mpira wa miguu. Tutaendelea kumkumbuka kwa heshima na kuthamini juhudi na upendo wake.

"Kifo chake ni pigo kwa familia yake na kwa jamii ya soka kwa ujumla," amesema Rais wa TFF, Wallace Karia.

Mwenyekiti wa DRFA, Lameck Nyambaya amesema, "marehemu alikuwa kiongozi mwenzetu, baba na mlezi wetu ambaye mchango wake katika utumishi wa DRFA na maendeleo ya soka utabaki kuwa kumbukumbu ya kudumu.”

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Ubungo (UFA), Carlos Sylivester amemtaja Daud Kanuti kama mtu aliyekuwa kiungo muhimu katika soka la mkoa wa Dar es Salaam.

"Huu ni msiba mkubwa sio kwa DRFA na Ilala pekee bali Tanzania nzima. Mikono ya Mzee Kanuti imelea na kusaidia wengi katika soka kuanzia wachezaji hadi viongozi. Hili ni pigo kubwa kwetu," amesema Carlos.