Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wema aja na DVD ya 'Heaven Sent'

Muktasari:

Dalili ya kuanza kulirudisha soko la filamu lililokuwa limelala, ambapo zamani wasanii ndio walizoeleka kwenda kuwapigia magoti wasambazaji.

Dar es Salaam. Baada ya kushinda tuzo ya msanii bora wa kike katika tuzo za filamu za ‘Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF)’, kupitia filamu yake  ya 'Heaven Sent', Wema Sepetu ameamua kuisambaza filamu hiyo kwa mfumo wa DVD.

Wema alisema mafanikio aliyoyapata tangu atangazwe mshindi, ni pamoja na utilianaji saini wa mkataba na kampuni ya Agusta itakayosambaza filamu hiyo.

Wema aliyekuwa ameongozana na Katibu muhtasi wake na mwandishi wa filamu hiyo aliyoshindia, Neema Ndepaya, alisema tangu aliposhinda kila mtu amekuwa na kiu ya kuiona filamu hiyo kwa kuwa alikuwa hajaiweka kwenye mfumo wa DVD.

Kutokana na uhitaji huo alisema sasa ameamua atafanya hivyo na kampuni tatu zilijitokeza kuomba kuwa wasambazaji, lakini ndio hivyo kisheria huwezi kufanya hivyo na kuamua kuichagua Agusta.

Wema alisema ni dalili ya kuanza kulirudisha soko la filamu lililokuwa limelala, ambapo zamani wasanii ndio walizoeleka kwenda kuwapigia magoti wasambazaji.

Naye Nemrice Soka, kutoka kampuni ya Agusta ambao ni wasambazaji filamu hiyo ya Wema, wamesema hii sio mara ya kwanza kufanya kazi na mrembo huyo na kukiri kuwa amekuwa akitengeneza kazi nzuri.

Hata hivyo aliwakaribisha wasanii wengine kupeleka kazi kwao kwani tofauti na wafanyabiashara wengine wao hawanunui hatimiliki ya msanii bali wanamuachia ili aweze kufadika nayo siku za baadaye.

Ndepaya mwandishi wa filamu hiyo, amesema wanashukuru nguvu kubwa waliyoitumia katika kuitengeneza filamu hiyo imezaa matunda kwani kuna wakati ilibidi warudi mara mbilimbili ‘location’.