Waziri Bashungwa atoa pole kwa Polisi Tanzania
Muktasari:
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ametoa pole kwa kikosi cha timu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara kilichopata ajali ya gari jana Ijumaa Julai 9, 2021 wakati kikitoka mazoezini katika Uwanja wa TPC, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, John Mapepele imesema kuwa “ Mh Bashungwa amehuzunishwa na taarifa ya ajali, Wizara inaungana na wapenzi wote wa michezo nchini kuwaombea mwa mwenyezsi Mungu majeruhi wote wapone haraka ili waendelee kutekeleza majukumu yao ikiwemo kumaliza michezo ya Ligi Kuu iliyobaki” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa msemaji wa timu hiyo, Hassan Juma, wakati ajali ikitokea gari la timu hiyo lilikuwa na watu 32 wakiwemo makocha, madaktari wa timu, na wachezaji.
Taarifa hiyoi imesema kuwa majeruhi wote wameruhusiwa kutoka kwenye Hospitali ya KCMC walikopelekwa aali na wanaendelea na matibabu katoika Hospitali ya Chuo cha Polisi Moshi isipokuwa Mshambuliaji Mathias Mdau ambaye bado yupo Hospitali ya KCMC akiendelea na matibabu.
Polisi Tanzania inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 42 na ilikuwa inajiandaa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliopangwa kuchezwa wiki ijayo katika Uwanja wa Ushirika Moshi.