Wabunge wafunika jukwaa kuu
Muktasari:
- Wakati mchezo wa Dodoma Jiji na Simba ukiendelea katika uwanja wa Jamhuri, wabunge wamekuwa sehemu kubwa ya watu waliofika hapo uwanjani.
Wakati mchezo wa Dodoma Jiji na Simba ukiendelea katika uwanja wa Jamhuri, wabunge wamekuwa sehemu kubwa ya watu waliofika hapo uwanjani.
Kuanzia kwa Godwin Kunambi wa Jimbo la Mlimba Morogoro, ambaye alishiriki vilivyo wakati wa timu kupanda ligi kuu, aliwaongoza wabunge kadhaa kuushuhudia mtanange huo.
Kunambi alionekana mara kadhaa akishangilia kwa kutembea mbele ya wabunge na watu wengine waliopo jukwaa kuu, wakati ambao wachezaji wa Dodoma Jiji walipokuwa wanakosa nafasi kwenye lango la Simba
Hamiss Mwinjuma (Mwana FA), Hamis Taletale (Babu Tale), Anthony Mavunde, ni miongoni mwa waliopo uwanjani katika jukwaa la watu mashuhuri wakifuatilia mchezo huo.