Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ujenzi wa viwanja Pemba wafikia pazuri

PEMBA Pict

Muktasari:

  • Kamishna wa Idara ya Michezo Zanzibar, Ameir Mohamed Makame amesema muda si mrefu viwanja hivyo vitakuwa na utaratibu wa kukabidhiwa. Amesema, Serikali imepanga viwanja hivyo vitumike kuwanufaisha wanafunzi na vijana kufanya mazoezi.

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Riziki Pembe Juma amesema ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa viwanja kisiwani Pemba.

Ameyasema hayo baada ya kukagua viwanja vya Wilaya ikiwemo Mkoani kilichopo Ukutini na Wete kilichopo Pandani.

Ameeleza, viwanja hivyo vipo katika hali nzuri na miundombinu rafiki kwa kila mtu kuanzia watoto, vijana na wenye ulemavu.

“Viwanja hivi vitatumika kukuza vipaji vya michezo mbalimbali na dhamira ya serikali vinufaishe wananchi kisiwani hapa,” amesema na kuwataka wananchi kuvitunza na kuvienzi ili vitumike kama ilivyokusudiwa na sio kinyume cha hapo.

Kamishna wa Idara ya Michezo Zanzibar, Ameir Mohamed Makame amesema muda si mrefu viwanja hivyo vitakuwa na utaratibu wa kukabidhiwa. Amesema, Serikali imepanga viwanja hivyo vitumike kuwanufaisha wanafunzi na vijana kufanya mazoezi.