Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uhuru bado kweupe, mashabiki wakijivuta Yanga Day

UHURU Pict

Muktasari:

  • Mashabiki wachache wameonekana wakifika uwanjani taratibu, huku maeneo ya nje ya uwanja yakiwa hayajajaa kama ilivyotarajiwa. 

HADI kufikia saa 6 mchana, hali ya Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambako Yanga inafanya tamasha lake la Yanga Day, kumekuwa na mwitikio mdogo wa mashabiki licha ya kuwepo kwa tangazo la mageti kufunguliwa saa 5 asubuhi.

Mashabiki wachache wameonekana wakifika uwanjani taratibu, huku maeneo ya nje ya uwanja yakiwa hayajajaa kama ilivyotarajiwa. Hata hivyo, hali hiyo inaweza kubadilika kadri muda unavyokwenda, hasa ikizingatiwa kuwa kilele chake itapigwa mechi inayotarajiwa kuanza saa 2 usiku.

Burudani mbalimbali tayari zinaendelea ndani ya uwanja, huku muziki ukisikika na kuwapa burudani mashabiki waliofika mapema. Pamoja na hayo, bado haijaonekana ile hamasa kubwa ambayo mara nyingi huambatana na matukio makubwa ya Yanga.

UHU 01

Uwanja wa Uhuru una uwezo wa kuingiza watazamaji 19,000 waliokaa, lakini hadi saa 6 mchana idadi ya waliofika ni ndogo. Mashabiki wengine wanaonekana kusubiri muda ukaribie zaidi ndipo waanze kuelekea uwanjani kwa wingi.

Yanga inatarajiwa kutumia tamasha hilo kuwatambulisha wachezaji wake wapya pamoja na kikosi kitakachotumika katika msimu ujao, huku burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali ikiwa sehemu ya tukio hilo.

Kwa sasa, macho yanaendelea kuwa kwa mashabiki hao wanaotarajiwa kuongezeka kadri muda unavyosogea.