Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ufinyu wa kikosi wamtesa Masoud Songea United

SONGEA Pict

Muktasari:

  • Masoud amesema timu hiyo ina wachezaji 16, baada ya wengine kushindwa kukamilisha taratibu zote za usajili katika dirisha kubwa lililopita, jambo ambalo limekuwa changamoto kwao ya kufanya vizuri kwa msimu huu.

KOCHA Mkuu wa Songea United ya Songea, mkoani Ruvuma, Juma Masoud amesema sababu ya mwenendo usioridhisha wa timu hiyo, ni kutokana na ufinyu wa wachezaji wa kikosi hicho, kwa sababu hadi sasa ana 16 tu, jambo linalochangia kufanya vibaya.

Masoud amesema timu hiyo ina wachezaji 16, baada ya wengine kushindwa kukamilisha taratibu zote za usajili katika dirisha kubwa lililopita, jambo ambalo limekuwa changamoto kwao ya kufanya vizuri kwa msimu huu.

“Ukiwaondoa wachezaji 11, wanaoanza benchi tunabakia na watano tu, hali hiyo ni mbaya sana kwetu kwa sababu tunashindwa pia kufanya mabadiliko ya mara kwa mara, jambo linalochangia wengi wao kukosa muda wa kupumzika vizuri,” amesema Masoud.

Masoud aliyejiunga na Songea United Januari 2026, akichukua nafasi ya Meja Mstaafu, Abdul Mingange.