Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amina Ally kurejea uwanjani

AMINA Pict

Muktasari:

  • Amina ambaye pia amewahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, alipata majeraha hayo wakati wa mashindano ya Ngao ya Jamii msimu wa 2024/25 katika mechi dhidi ya Yanga Princess, hali iliyomweka nje ya uwanja na kuanza safari ya matibabu.

KIUNGO wa zamani wa Yanga Princess, Simba Queens na JKT Queens, Amina Ally amesema ana matumaini ya kurejea uwanjani mwakani au dirisha dogo la usajili na bado yupo kwenye hatua za kupona majeraha ya goti na mkono aliyoyapata akiwa Simba Queens.

Amina ambaye pia amewahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, alipata majeraha hayo wakati wa mashindano ya Ngao ya Jamii msimu wa 2024/25 katika mechi dhidi ya Yanga Princess, hali iliyomweka nje ya uwanja na kuanza safari ya matibabu.

Akizungumzia na Mwanaspoti kuhusu hali yake, kiungo huyo amesema awali alipelekwa hospitalini baada ya kuumia na alitibiwa mkono na baadaye kufanyiwa upasuaji wa goti.

"Nilipata majeraha ya goti na mkono kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga. Nilipoenda hospitalini nilianza matibabu ya mkono na baadaye nikafanyiwa upasuaji," amesema Amina.

Ameongeza wakati akipata majeraha hayo alikuwa bado ana mkataba na Simba Queens, lakini ulipomalizika hakuongezewa mkataba mwingine, wakati huo akiwa bado anaendelea na matibabu na kuuguza majeraha yake.

Pamoja na changamoto hiyo, Amina amesema anaendelea kufuatilia maendeleo ya afya yake kwa ushauri wa daktari, ambaye amemweleza ndani ya miezi miwili ijayo anaweza kuanza mazoezi mepesi.

Akizungumzia matarajio yake, kiungo huyo amesema anaamini anaweza kurejea uwanjani mwakani au wakati wa dirisha dogo, kutegemea maendeleo ya kupona kwake.

Hata hivyo, kurejea kwake kutategemea tathmini ya kitabibu na uwezo wake wa kurejea kwenye mazoezi bila kuhatarisha afya yake.