Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tusker yajitoa Kagame, Yanga wapewa Malawi

TIMU ya Tusker inayoshiriki Ligi kuu ya Kenya imejiondoa katika michuano ya Kagame kwa ukanda huu wa Afrika mashariki na kati yanayotarajiwa kuanza Agosti Mosi - 14, Jijini Dar es Salaam.

Kufuatia kujitoa kwa timu hiyo ni muendelezo wa timu kadhaa ambazo zimefanya hivyo ikiwemo mabingwa wa Tanzania Bara Simba, na APR ya Rwanda.

Hatua hiyo inaifanya kamati ya mashindano ya CECAFA kubadilisha makundi huku timu nne zikiwa katika makundi mawili.

Timu ya Uganda Express FC wataanza mechi yao ya kwanza dhidi ya Atlabara FC kutoka Sudan Kusini Agosti mosi huku Yanga ikipambana na Nyasa Big Bullets FC ya Malawi.

Yanga awali ilipangwa kucheza na Expres ya Uganda katika mechi yao ya kwanza.

Yusuf Mosi, ambaye ni muuongozaji wa michuano ya CECAFA alisema kuwa michuano hiyo itatumika katika viwanja vya Benjamin Mkapa na Azam Complex Chamazi.

“Tunategemea mashindano yenye ushindani huku timu bora kutoka kila kundi ikienda moja kwa moja hatua ya nusu fainali' hii itasaidia pia timu kujiandaa vyema kueleka michuano ya (CAF) inayotarajiwa Septemba" alisema

KCCA FC ya Uganda ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo baada kushinda mwaka 2019 nchini Kigali Rwanda.

Kundi A: Young Africans (Tanzania), Nyasa Big Bullets (Malawi), Express FC (Uganda), Atlabara FC (South Sudan)


Kundi B: KCCA FC (Uganda), Azam FC (Tanzania), Le Messager Ngozi (Burundi), KMKM FC (Zanzibar).