Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tunawezesha Taifa

Mtendaji mkuu wa zamani wa Campbell Soup, Doug Conant aliwahi kusema: “Ili kufanikiwa sokoni, ni lazima kwanza ufanikiwe kazini.”

Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) inafanya mageuzi kutoka kuwa mchapishaji wa magazeti na kuwa kampuni kamili ya huduma za kidigitali, ikiwapa thamani wateja wake tofauti:

Hawa ni pamoja na wasomaji wanaotutafuta kwa ajili ya habari na maoni, wachapishaji wanaochapisha kwetu, watangazaji wanaotangaza bidhaa zao nasi na wateja wetu wa mashirika na taasisi wanaotuamini tuwajengee taswira njema kwa umma.  Kwa MCL, kufanikiwa sehemu ya kazi,  huanza na lengo lililoelezewa kifasaha na watu walioshirikishwa kikamilifu ambao wanatumia utamaduni na michakato inayotufanya tuwe wanyumbufu, wasikivu na  taasisi inayojifunza. Kufanikiwa sokoni hufuatiwa na bidhaa zilizo na utofauti ambazo humpa thamani mteja wetu ndani na nje ya biashara ya habari.

Lengo letu, lililoelezewa kwa ufasaha, ni kuwezesha jamii inayotuzunguka kupitia maudhui na huduma zetu.

Kaulimbiu yetu mpya: “Tunawezesha Taifa” ambayo ni  ya kwanza katika miaka 23 ya kampuni yetu,  inaakisi ahadi hiyo. MCL imeundwa ili kuwezesha jamii inayotuzunguka na kuiletea mabadiliko chanya.

Hatua yetu ya kuanzia ni kuupa maana mpya uandishi wetu wa habari. Ni lazima tuwe na nia zaidi katika kile tunachoripoti na jinsi tunavyoripoti.

Tunakusudia kuachana na  kuwa mabingwa wa kuelezea matatizo, tukilenga kujikita katika uchambuzi kuanzia katika kuelezea matatizo hadi kutoa suluhisho linalotokana na utafiti,ili  kusukuma ajenda ya maendeleo na kuonyesha matokeo.

Tunaendelea kuboresha majukwaa yetu ya habari na taarifa. Tunazingatia utofauti na kuongeza uwakilishi kuanzia wanawake, vijana hadi makundi mbalimbali ya pembezoni yanayosahaulika.

Kwa dhamira kubwa, tunapaza sauti za wasio na sauti, na tunafanya hivyo bila kuchoka. Hivi ndivyo tunavyowezesha wateja wetu. Hivi ndivyo tunavyowezesha Taifa.

Tunaiweka wazi ahadi yetu kwenu, kwa sababu tunataka ninyi wasomaji wetu, mtuwajibishe. Tunapoendelea kukuza biashara zetu, kuanzia mfanyakazi mmojammoja hadi kampuni nzima, tunataka mtarajie makubwa kutoka kwetu na mtukosoe tunaposhindwa kufikia matarajio hayo.

Kama wachapishaji wa Mwananchi, The Citizen, Mwanaspoti, Mwananchi Digital, Mwananchi Scoop na majukwaa mengine katika mitandao ya kijamii, tunaitambua fika nguvu ya kuwa na taarifa sahihi.

Ahadi yetu ni kuendelea kukuwezesha kwa kukupa taarifa zinazokusaidia kufanya maamuzi ukiwa na ufahamu, kuona na kutumia fursa, kutambua hali inavyokwenda duniani na hapa nchini na kujifunza.

Tutaendelea kukupa taarifa, kukuelimisha na kukuburudisha, lakini tunaahidi kufanya hivyo kitofauti. Uandishi wetu utakuwa wa kuchunguza na wenye kutoa suluhisho.

Tunapokupa taarifa, itakuwa kwa madhumuni ya kukuwezesha kufanya maamuzi sahihi. Tunapoelimisha, tutakuonyesha fursa zilizopo na kukuhamasisha kuona namna ya kuzivumbua na kuzitumia fursa hizo. Tunapokuburudisha, tutazingatia maadili ambayo yataifanya Tanzania na Watanzania wawe na muonekano chanya.


Maudhui yetu yatayapa nguvu maisha yako

Tukiwa kama taasisi ya huduma za kidijitali katika karne ya 21 yenye biashara zaidi ya habari, MCL pia itakuwezesha kwa kukuletea thamani kupitia shughuli zake nyingine kama vile:

Majukwaa yetu ya fikra (Thought-Leadership Forums.) yatakayotujengea ufahamu kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa na kuhusisha katika mijadala.

Vitengo vyetu vya matangazo na usambazaji magazeti, dijitali na maudhui mengine, vitakutanulia wigo wa kibiashara na kukuwezesha kufikia wateja wengi zaidi.

Huduma yetu ya uchapishaji itakupa ubora wa kipekee na kuwezesha wateja wako wauone ujumbe wako kwa utofauti.

Huduma yetu ya usafirishaji vifurushi itakufikishia bidhaa zako kwa wateja kwa wakati na kukuwezesha kukuza biashara yako.

Kitengo chetu cha Habari Hub kitakuza na kuwezesha mawazo na ubunifu wako.

Tumejipanga upya kwa kuweka watu sahihi katika nafasi sahihi na kumwezesha kila mmoja kukuletea maudhui yanayogusa maisha yako, bidhaa na huduma zinazotupa kipato na ubunifu ili kukuza biashara.

Azma yetu Mwananchi ni kujenga utamaduni wa pamoja, unaoainisha maana ya kuwa Mwana-MCL, na tunachopaswa kufanya kuwezesha hadhira na wateja wetu.

Timu zetu zimehamasika, ziko tayari. Tunaendelea kushirikiana na mkakati tunao. Tuko tayari kufanikiwa na kushinda katika soko.

Chachu ya mabadiliko yetu ni uandishi na uanahabari wetu. Hivyo basi, mapinduzi yetu ya kibiashara hayamaanishi kwamba tutaacha uchunguzi.

Kiu yetu ya mapato haimaanishi tutaangalia upande mwingine pale uozo unapojitokeza.

Tunaahidi kujikita zaidi kuripoti habari kuhusu  utawala bora (good governance),   tukiwa vinara wa kuchambua ajenda za kitaifa na kimataifa na kuzipa maana katika maisha yako.

Tutafanya hivyo kwa usawa, bila kuegemea upande wowote, na kwa namna yenye uwiano, tukihakikisha tunakuletea habari kamilifu kila wakati. Huo ndio msingi wetu wa Ki-Mwananchi. Hivyo ndivyo sisi Wana-MCL #tunawezeshataifa.

 Bakari S. Machumu

Ofisa Mtendaji Mkuu, Mwananchi Communications Ltd.

LinkedIn: Bakari S Machumu

Twitter: @bmachumu


MWANANCHI IKO MSTARI WA MBELE KUTUELIMISHA

"Sisi wote ni mashahidi kwa namna ambavyo kampuni ya Mwananchi imekuwa ikielimisha jamii, kupitia vyombo vyake na imekuwa ikitusaidia sana katika kuhakikisha nchi yetu inaendelea. Serikali tunajenga uchumi wa kidijitali, uchumi ambao kila mmoja anaweza kushiriki; tunafurahi kuona nanyi mnafanya bunifu mbalimbali za kiteknolojia na leo mmekuja na ubunifu huu,  huku ndiko tunakoelekea hivyo ushirikiano huu utakuwa na matokeo mazuri

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Jim Yonazi


AHADI YETU KUSUKUMA MAENDELEO NCHINI

"Nafurahi kuona Mwananchi ikizidi kukua. Nakumbuka tulikuja hapa kufuatia mwaliko wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa. Tulikutana naye na baada ya majadiliano tukafikia kuanzisha kampuni ambayo kwa sasa tunaweza kujivunia inafanya vizuri kwenye sekta ya habari, na ahadi yetu ni kuendelea kulisukuma gurudumu la kuhabarisha umma.”

Mwenyekiti  wa Bodi ya NMG, Dk Wildfred Kiboro


MABADILIKO SAHIHI KWA MAHITAJI YA JAMII

"Mabadiliko yataendelea kufanyika ili kwenda sawa na mahitaji ya jamii. Sasa hivi watu wengi hawana utamaduni wa kusoma magazeti hasa vijana, kwani wanasema wana namna zao za kupata taarifa na hapa ndipo teknolojia inapokuja,  hivyo ni lazima tubadilike kwenda na kasi hiyo kwa kuwa wabunifu kuwafuata huko waliko ili tusiwakose."

Mwenyekiti wa Bodi ya Mwananchi Communications Ltd


TUNAAKISI MAISHA YAKO

Simulizi tamu hubadilisha maisha yako. Waandishi wabunifu, kutoka Oscar Wilde (The Importance of Being Earnest) mpaka Sue Monk Kidd (The Secret Life of Bees) wanalitambua hilo siku zote.

Hutasahau simulizi tamu, kwani zinakugusa, na unatembea nazo moyoni kila uendapo. Simulizi hizo hujaa hisia na uhalisia; zinakuna nafsi yako na kukupa msukumo wa kuchukua hatua.

Nia yetu kubwa kama Mwananchi Communications Limited (MCL) ni kukuletea simulizi tamu kupitia uandishi wetu wa habari.

Tutakuonyesha suluhisho na uwazi pale vinapokosekana, tutahoji yale yasiyoeleweka, tutashangilia mafanikio yanapojidhihirisha na kuuliza maswali magumu pale mamlaka zinapokusahau.

Maudhui yetu yatawezesha maisha yako, yatabeba changamoto zako, na kukuhamasisha ufanikiwe maishani, kazini na katika biashara zako; unapoongoza na unapoongozwa.

Fasihi simulizi ni tunu ya taifa letu; ni sehemu ya utamaduni wa hadithi wa Kiafrika.

Hapo kale, babu na bibi zetu walikusanyika kuota moto na kusikiliza hadithi kuhusu dunia inayowazunguka, ili kujifunza, kukuza fikra zao, kuongeza uelewa, kurekebishana na kubadilishana mitazamo yenye kuleta suluhisho na tija.

Hii ndiyo ahadi yetu kutoka vyumba vya habari vya MCL. Tutakuletea maudhui yanayokidhi mahitaji yako kama mtu binafsi, kampuni, taasisi na kama taifa lenye kiu ya mafanikio na fikra chanya.

Uandishi wetu utaakisi ukweli wako, na kukuwezesha kufanya maamuzi sahihi, kutoa thamani kwa wateja wako na kushawishi wenye mamlaka wafanye maamuzi yanayolinda maslahi yako.

Tutasimulia maisha yako. Tunapofanya hivyo, #tunawezeshataifa.

Victor Mushi

Mhariri Mtendaji Mkuu, MCL

LinkedIn: Victor Amani Mushi

Social: @victraman (TWTR, IG)


MAUDHUI SAHIHI KWA WAKATI, UAMUZI SAHIHI

Miaka 23 ya Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd imekuwa na mafanikio makubwa katika utekelezaji wa sera yake ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Utekelezaji huo umefanyika kupitia maudhui yaliyopitishwa na kuchujwa na jopo la wanataaluma waliobobea katika tasnia ya habari huku yakizingatia mizania yenye haki na usawa.

Kupitia gazeti la Mwananchi na mitandao yake ya kijamii, maudhui yetu yamechochea mabadiliko katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na kijamii na kusaidia harakati za taifa letu kusonga mbele kimaendeleo.

Baada ya mafanikio hayo, sasa tuko tayari kubeba sera, utamaduni, lugha yetu adhimu ya Kiswahili na haiba ya Mtanzania, na kuzitangaza kitaifa na kimataifa.

Ndio maana tunasema, tunawezesha taifa kufikia malengo na utekelezaji wa mikakati mbalimbali na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo, tukiaminika kwa kubeba ajenda kubwa za kitaifa.

Tutafanya haya kupitia maudhui yetu ndani ya gazeti la Mwananchi na mitandao yake ya kijamii, kuwawezesha Watanzania kupata habari zenye tija kwa wakati sahihi ili kufanya uamuzi sahihi wenye tija kwa mustakabali wa maisha ya mtu mmojammoja na Taifa letu.

Tunawezesha taifa kwa kujikita kwenye habari zitakazoleta matokeo chanya ili kuwezesha jamii ipate uelewa wa kutosha na kupata mwelekeo sahihi.Tunawezesha taifa kwa kuchapisha habari zilizochambuliwa kwa kina, zinazozingatia kutoa suluhisho la changamoto au matatizo yanayoikabili jamii.

Tunatambua wajibu wetu wa kuelimisha, kuburudisha na kuhabarisha jamii, hivyo malengo yetu yatajikita zaidi katika kumwezesha msomaji na wadau wetu kupata maarifa mapya, mbinu na suluhisho katika kufikia uamuzi sahihi.

Kama Mhariri Mtendaji wa gazeti linaloongoza nchini na linalowafikia watu wa mijini na vijijini, nawaahidi wasomaji wetu kwamba, maudhui yetu yatajikita eneo hilo na tutatekeleza ahadi hii kwa vitendo kwa masilahi mapana ya Tanzania. #tunawezeshataifa.

Joseph Damas

Mhariri Mtendaji, Mwananchi

Social: @JosephDamas2 (TWTR); @jdamas_ (IG)


MAUDHUI YANAYOJIBU CHANGAMOTO ZAKO

Mwananchi Online inawezesha Taifa kwa kuchochea maendeleo na utawala bora nchini kupitia tovuti, mitandao na majukwaa yake mbalimbali. Katika kutimiza lengo kuu la Mwananchi Communications Limited (MCL) la kuwezesha jamii tunazozifikia kupitia maudhui na huduma zetu, tunaahidi:

Kutoa maudhui yatakayotoa majawabu ya changamoto za jamii: Kupitia jukwaa hili tutaandaa maudhui yanayompa nafasi msomaji na mtazamaji kujua njia sahihi za kupambana na changamoto zinazomkabili. Kukosoa kwa weledi na kutoa nafasi kwa mamlaka kutoa ufafanuzi: Maudhui yote yatajikita kwenye weledi hasa tunapokosoa, na tutatoa nafasi kwa mamlaka husika kujibu na ikiwezekana kuwaonyesha njia ya kutokea.

Kuwezesha majadiliano (Two-way communication) kwenye mitandao ya kijamii: Tunawezesha taifa kwa kuwapa fursa wasomaji na watazamaji wetu kutoa maoni yao, kuyasikiliza na kuyafikisha mahali husika kwa ajili ya kutatua changamoto za wananchi.

Ili kuchochea mawasiliano kwa maendeleo, tunadhamiria kufanya maudhui yenye tija kwa maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla ili kuleta chachu kwenye jamii, na maudhui hayo yatagusa aina zote za watu kuanzia wenye kipato cha chini, cha kati na cha juu.

Kukuletea taarifa sahihi kwa uthabiti: Tutaendelea kuwa chombo kinachowapa wasomaji na watazamaji uhakika wa maudhui yanayosambaa mitandaoni, kwa kujenga mifumo thabiti ya ufuatiliaji na uhakiki wa taarifa tunazochapisha ama kurusha kupitia majukwaa yetu. #tunawezeshataifa.

Zourha Malisa

Kaimu Mhariri Mtendaji,

Online & New Content

LinkedIn: Zourha Malisa

Social: @ZourhaMalisa (TWTR), @zourha (IG)


HABARI AMBAZO NI MUHIMU KATIKA BIASHARA NA ZAIDI YA HILO

Gazeti la The Citizen lina jukumu muhimu kama chanzo cha kuaminika cha habari za biashara nchini Tanzania na kama daraja kati ya Serikali, watu linaowahudumia, na jumuiya ya kimataifa.

Kupitia habari tunazosimulia na habari tunazoandika kwenye magazeti na dijitali tunawezesha jumuiya ya wafanyabiashara, mashirika na sekta ya kibinafsi kwa pana zaidi.

Pia tunawezesha kizazi kinachokua cha wavumbuzi na wajasiriamali kwa kushiriki na kuripoti habari zao za matamanio na kupiga hatua kupitia mifumo kama vile SMEs Digest na Jarida letu la kila wiki la Success Magazine.

Pia tuna nia ya kuziba pengo la kijinsia katika uongozi wa kisiasa na ushirika, katika taaluma, na katika nyanja zingine. Kwa hivyo, tunawezesha wanawake na kusherehekea mafanikio yao kupitia mpango wetu wa kila mwaka wa The Citizen Rising Woman Initiative.

Gazeti la The Citizen si tu la kuwezesha wasomaji wake bali Tanzania nzima kama taifa kwa kutumika kama ghala la taifa la data na habari zozote za kisekta zinazoweza kufikiwa na jumuiya ya kimataifa. Hii ni sehemu ya njia yetu ya kimkakati ya maudhui ya uhariri inayoitwa ‘The gateway of Tanzania to the world’ (Lango la Tanzania kwa ulimwengu).

Kupitia mpangilio wa maudhui ya ajenda tunaunda mazungumzo ya kitaifa yenye matokeo na kupigia debe masuluhisho ya masuala ambayo ni muhimu zaidi kwa Watanzania. #tunawezeshataifa.

Mpoki Thomson

Mhariri Mtendaji, The Citizen

LinkedIn: Mpoki Thomson

Kijamii: @Mpokithoms (TWTR), @Tanzanianjourno (IG)


SISI NI INJINI INAYOONGOZA MAENDELEO

Gwiji wa Yoga, Sadhguru anasema: “Taifa si ardhi na majengo yake ni watu wake.” Iwapo sisi kama taifa itabidi tuinuke na kuwezeshwa, jambo la kwanza tunalotakiwa kufanya ni kuwezesha wananchi.

Katika masuala ya fedha, tunawezesha rasilimali kubwa zaidi ya MCL: mtaji wake wa kibinadamu. Tunawawezesha wengine katika taasisi kufanya uamuzi ambao utaleta thamani bora kwa wateja na kukuza kampuni. Watu ndio nyenzo yetu muhimu zaidi: wao ndio kisima cha fikra kinachoendesha mkakati. Nadharia ya Maslow inasema mahitaji yetu yanaamuru tabia. Kuelewa kile ambacho watu wanahitaji hutengeneza msingi wa kuwatia moyo. Fedha ina jukumu muhimu katika kupata riziki, kwa kuhakikisha kuwa kuna mwendelezo katika biashara. Tunaweka vidhibiti vinavyofaa vinavyowezesha kila mtu kufanya uamuzi sahihi. Tunachochea biashara, na kuhakikisha MCL inastawi licha ya usumbufu unaosababishwa na mabadiliko ya teknolojia. Fikiria fedha kama tanuru la kampuni ya chuma, kudumisha halijoto bora (michakato) ili kuhakikisha bidhaa inafika sokoni, inakidhi mahitaji ya wateja na kuzalisha mapato kwa kampuni.

Tunaishi katika ulimwengu ambapo watu binafsi na biashara lazima ziendelee kukua, kuwa anuai na kubadilika ili kukidhi mahitaji yao wenyewe na kubaki kuwa muhimu sokoni.

Kama kiongozi, ninahakikisha kila mtu katika MCL anajiona kama mali muhimu kwa taasisi, bila kujali changamoto hizi. Hiyo ni hatua yangu ya kuwezesha.Dhamira yetu ya pamoja ni mwendelezo wa biashara. Kwa pamoja, tunaliwezesha Taifa kwa MCL kuwa kama kampuni ya vyombo vya habari, huku tukilinda mustakabali wake kama kampuni ya huduma mbalimbali za kidijitali.

Amos Simiyu

Meneja wa Fedha, MCL

LinkedIn: Amos Simiyu


KUWEZESHATAIFA: KUONGOZA KWA MATOKEO

Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inabadilika kutoka uchapishaji wa magazeti hadi kuwa taasisi kamili ya huduma za kidijitali, na kutoa thamani ya maana kwa wateja wake mbalimbali.

Rasilimali Watu ndiyo kichocheo kikuu cha mabadiliko hayo, kuhakikisha MCL ina wafanyakazi sahihi ambao huisaidia kutambua maono yake ya kuwezesha taifa kwa kutoa uandishi wa habari wenye matokeo, wenye mwelekeo wa ufumbuzi, na thamani kwa wateja katika biashara zetu nyingine.Katika rasilimali za kibinadamu za MCL, tunaamini katika uwezo wa mtu binafsi wa kuleta matokeo ya maana na ya pamoja. Tunaliwezesha taifa, kwa kuwawezesha wale wanaofanya kazi nasi. Tunazingatia ubora, na kujenga viongozi wa baadaye.

Tunaajiri watu wanaofaa katika kazi zinazofaa ili kuendesha utendaji unaofaa wa biashara. Tunalinganisha ujuzi na majukumu, na kuhakikisha kila mtu katika taasisi anafanya kazi kwa lengo moja, anachangia malengo ya kampuni, na kwa njia yake mwenyewe, anahudumia jamii pana.

Tunafanya kazi kwa bidii kuwahifadhi wale wanaoshiriki malengo yetu, na kuwasaidia kujifunza, kupanua upeo wao na kukuza taaluma zao. Tunajihesabu kama mwajiri bora wa Tanzania: uwanja wa kuthibitisha ubora, ambapo anga ni kikomo.

Tunajenga maelewano ya mahali pa kazi ambayo yanaruhusu wanahabari wetu, watu wetu wa masoko,

Hayo ndiyo matokeo yetu katika jamii. Ndivyo tunavyoliwezesha taifa.

Paul Hamidu, Meneja Rasilimali Watu, MCL

LinkedIn: Paul Hamidu


KWA USHAURI NA UKUAJI WA BIDHAA ZETU SOKONI

Malala Yousafzai aliwahi kusema “Ninapaza sauti yangu—si ili niweze kupiga kelele, bali ili wale wasio na sauti wasikike. Hatuwezi sote kufanikiwa wakati nusu yetu inasita.”

Kitengo cha masuala ya biashara na masoko ndicho chombo kikuu cha mawasiliano kwa bidhaa zote za MCL. Tunaunganisha usimamizi wa wenye sifa njema, kujenga uhusiano na shughuli zinazolengwa ili kusaidia utoaji wa kibiashara kwa bidhaa zetu, washauri na ukuaji wa kibinafsi.  Tangu kuanzishwa kwake, bila kuchoka MCL imekuwa ikitafuta usahihi na uvumbuzi, ikiwezeshwa na hekima ya zamani na ufahamu thabiti wa siku zijazo. Mbali na rajamu, MCL ni lango la maarifa, yenye teknolojia ya ubunifu, kulisha umma dara za hali ya juu, kutafuta suluhu ya matatizo, utafiti wa kitaalamu, uandishi wa habari ulioshinda tuzo, programu zinazoweza kugeuzwa kukufaa na mifumo ya uwasilishaji ili kuleta taarifa muhimu kwa wateja wake, lini na mahali wanapozihitaji kila siku.

Tuna desturi nzuri za kutoa mrejesho na kuhakikisha wafanyakazi wanapata fursa ya kutumikia jamii zao. Tunatetea utamaduni jumuishi na wenye usawa na kujitahidi kuvutia na kuwaendeleza wafanyakazi wenye vipaji.  Mkakati wetu kuandaa bidhaa zenye ubora, upekee na za aina mbalimbali ili kuvifikia vikundi vinavyolengwa, kuwa na ushindani, kuwa na mikakati bunifu na inayoweza kunyumbulika ya uuzaji, kuwa na timu yenye ufanisi na iliyowezeshwa, na kufanya biashara kwa mujibu wa kanuni za utawala bora wa taasisi. Tutafanya shughuli zetu kwa maadili, heshima na kuwajibika mkubwa .

Vivian S Temi- Meneja masoko

Corporate Affairs & Marketing Manager, MCL

Linkedin: Vivian Temi


TUNAWEZESHA MAMBO MAZURI

Tunawezesha Taifa. Ndio kaulimbiu mpya ya Mwananchi Communications (MCL). Kaulimbiu hiyo inabeba dhamira kubwa ya MCL, wachapishaji wa Mwananchi, Mwanaspoti, The Citizen na Mwananchi Digital kwa jamii ya Tanzania, Afrika na dunia kwa ujumla.

Katika Mwanaspoti, dhima hiyo itatekelezwa kinagaubaga kupitia kazi zetu za kila siku ambazo ni kuelimisha,kuburudisha, kukosoa na kutoa suluhisho katika mambo mbalimbali ya michezo na burudani.

Timu ya Mwanaspoti, gazeti la Kiswahili la michezo linaloongoza zaidi sio Tanzania tu, bali pia Afrika Mashariki, inaahidi kuliwezesha taifa kupitia kazi zetu ambazo sasa tunakwenda kuziboresha zaidi. Tunatambua kwamba jamii ya wanamichezo imetupa heshima kubwa kwa kutuamini kuwa sisi ndicho chanzo chao kikubwa cha kuaminika cha habari.

Ahadi yetu kwao ni kuendelea kulinda heshima hiyo kwa kuongeza wigo wa habari, makala na uchambuzi kila siku katika michezo na burudani kwa kuzingatia ubunifu na weledi.

Ombi letu kwenu ni kuendelea kutuunga mkono kwa kuendelea kututegemea kama chanzo chenu kikuu cha habari za michezo na burudani,lakini pia kutupa mrejesho wa kazi zetu ili tuendelee kuwaletea maudhui yanayoendana na matakwa yenu.

Tukishirikiana katika hilo, kwa pamoja tutakuwa tumetiza dhamira yetu ya #kuwezeshataifa.

Michael Momburi

Mhariri Mtendaji, Mwanaspoti

LinkedIn: Michael Momburi


TUNAFIKA, KILA MAHALI

Kitengo cha Ubunifu na Usaidizi wa Kidijitali (DIS) huwezesha taifa kwa kutingisha hali iliyopo na kuleta mawimbi ya mabadiliko katika sekta zote. Udakizaji unaodhibitiwa ni muhimu kwa maendeleo ya jumla ya taasisi yoyote.

Kupitia HabariHub, MCL inaendelea kusukuma fikra na bidhaa za kisasa kuingia sokoni na kubadilisha jinsi shughuli za kila siku zinavyofanyika ndani na nje.

DIS katika MCL inaongoza kwa udakizaji huo, inairasimisha kuwa mkondo thabiti wa ukuaji, na kuipa utaratibu na muundo wa kupatana na miundo ya kitamaduni ya biashara ambayo tumeizoea pia. Tunawezesha taifa kwa kuendeleza teknolojia za kidijitali ambazo zinaweza kutumika na kuongezwa kwa njia endelevu ili kuruhusu wachapishaji na waandaaji maudhui kuungana na hadhira zao, na kupata mgawo wa pato katika hali ya kiuchumi inayobadilika kila mara. DIS pia inakuza ushirikiano usio wa kidesturi ambao huunda mitandao muhimu katika sekta na tasnia tofauti, ili kuruhusu kampuni za vyombo vya habari kustawi katika zama za kidijitali ambazo hutegemea sana hisia za watumiaji, uwasilishaji na maudhui yasiyopitwa na wakati.

Kwa kujumuisha miongo, vizazi na jumuiya ambazo zimeunganishwa na kanuni za kawaida, DIS inahakikisha maudhui ambayo yanayotolewa si tu kuwa yanafaa, sahihi na ya kweli, bali yanafika kwa wingi zaidi ndani na nje ya mipaka ya kitaifa. Hii inajenga ulimwengu wenye usawa na unaoshirikishwa kwa kuhakikisha zinafika popote pale mtu alipo. Hivyo ndivyo #tunavyoliwezesha taifa.

Mihayo Wilmore

Digital & Innovation Lead, MCL

LinkedIn: Mihayo Wilmore


KUFAHAMISHWA NI KUWEZESHWA

Habari ni nguvu (uwezo). Kama kampuni ya maudhui, jukumu letu ni kuhakikisha mwananchi wa kawaida anapata taarifa muhimu kupitia majukwaa ya habari yaliyothibitishwa ili kuwasaidia kuwa raia bora wanaojitahidi si tu kujiendeleza, bali kuliwezesha taifa kwa ujumla.

Tangu usajili wetu miaka 23 iliyopita, wasomaji wetu wamepokea habari zinazotegemeka kupitia machapisho na majukwaa yetu ili kuwasaidia kufanya uamuzi sahihi katika maisha na kazi zao. Kwa chumba chochote cha habari kote ulimwenguni, hayo ndiyo mafanikio makubwa zaidi.

Matokeo huonekana kila mara habari za uongo zinaposambazwa na wasomaji hawajui wa kumtegemea. Wale wanaohisi wamepotea au kukosa habari zinazowapa uwezo, wamegeukia MCL ili kupata taarifa sahihi. Sisi ni suluhisho kwa Taifa.

Tunatoa mwanga, tunafungua macho ya wengi ili waweze kuona vizuri. Tunawasilisha maudhui muhimu katika maisha ya kila siku. Tunasimulia hadithi nyingi ambazo hazijasimuliwa, tunaboresha maisha yaliyoachwa, na kuwawezesha wengi kufikiri tofauti tunapokumbatia ujumuishaji na utofauti katika kazi yetu.

Tunatoa huduma za thamani na zilizoongezwa thamani ndani ya mifumo yetu. Tunapowasilisha thamani hiyo, kipaumbele chetu ni kuhakikisha maudhui yetu hayakiuki haki za wengine, hayakashifu sifa za wengine, yanawapa wengine haki ya kusikilizwa kabla ya kuchapishwa, na kwamba tunapofanya makosa, tunawajibikia na kuwaomba msamaha wale ambao tumewadhuru.

MCL ni hazina kubwa ya maarifa. Kuripoti taarifa za kuaminika ni dhamira yetu. Ndivyo tunavyoliwezesha Taifa.

Josephat Kesagero

Meneja Sheria na Utawala, MCL

LinkedIn: Josephat Kesagero

Instagram: Josephat Kesagero


UJUMBE SAHIHI, NJIA SAHIHI, MTEJA SAHIHI

Mzee kipofu ameketi kwenye kona ya barabara yenye shughuli nyingi katika njia ya waenda kwa miguu, akiomba mabadiliko. Ana alama ya kadibodi karibu na kikombe kitupu cha bati. Ishara inasema: “Kipofu, tafadhali nisaidie!” Lakini hakuna mtu anayempa pesa yoyote.

Mwandishi mchanga mtangazaji anapita na kumwona yule kipofu, akiwa na ishara yake, na kikombe chake kitupu cha bati. Anawaona watu wengi wakipita na hawamtambui mzee huyo. Anajisikia vibaya na anataka kusaidia. Mwandishi anafikiri kwa muda, anatoa kalamu yake ya alama, na kuandika kwenye ishara. Kisha anaweka pesa kwenye kikombe chake na kwenda zake. Kwa muda mfupi, watu wengine wanaanza kuweka pesa katika kikombe.

Bati linajaa haraka sana, na kuzidi. Yule kipofu, akistaajabishwa na ukarimu huo wa ghafla, na akikumbuka mwandikaji akiandika, anauliza mtu asiyemjua anayepita, “Je, unaweza kunisomea ishara hii?” Mgeni huyo anasoma, “Ni siku nzuri. Unaweza kuiona. Siwezi.”

Kama kampuni ya habari, Mwananchi Communications Limited (MCL) inaliwezesha taifa kama vile mwandishi alivyomwezesha kipofu. Tuna watazamaji wengi katika bidhaa za uchapishaji na dijitali. Hadhira hii inahitaji kukuelewa. Lazima uwe na ujumbe sahihi, katika njia sahihi, na lazima uwafikie wateja wako watarajiwa popote walipo. Katika kitengo cha kibiashara cha MCL, tunakusaidia kuwasilisha ujumbe unaofaa kwa hadhira inayofaa kupitia njia zinazofaa.

Nyayo zetu zinajumuisha majukwaa ya uchapishaji na dijitali, matukio na mabaraza, yenye mazoezi ya ushirikiano yanayokua kila mara. Tunakusaidia kuweka pamoja ujumbe wa ushindi unaokuza rajamu yako, bidhaa zako na masoko yako. Tunakuletea mbele ya wateja wako.

Tunaiwezesha biashara yako, na kwa pamoja, tunawezesha taifa.

Mugabe Kenneth Bagonza

Mkuu wa Kitengo cha Biashara, MCL

Unganisha: +255 767 131 330


HUDUMA YA THAMANI, KIFURUSHI KWA WAKATI, TOLEO KWA WAKATI

Katika Mwananchi Courier na uchapishaji, tunafanya miunganisho ambayo inaleta thamani kwa watu binafsi na mashirika. Ndivyo tunavyoliwezesha taifa.

Huduma yetu ya usiku ya kusafirisha vifurushi huunganisha familia, bidhaa kwa watumiaji wa mwisho, makampuni na wateja. Tunarahisisha usafirishaji wa bidhaa na huduma kutoka sehemu A hadi sehemu B. Baba mmoja wa Mbeya anapotaka kuipelekea familia yake Dar kilo 20 za mchele tunafanya hivyo. TV mpya kwa mteja wako wa Mwanza? Tutakuletea hapo ulipo! Nyaraka muhimu kutoka kwa wakili wako huko Dar? tutawaletea.

Tunakusaidia kubaki na wateja wako, kwa sababu ukiwa na Mwananchi Courier, unaweza kuwahakikishia kuletewa bidhaa mara moja. Tunapanua wigo wako wa soko, kwa kuwezesha ufikiwaji wa saa 24 kwa kila mkoa Tanzania. Kwa kusafirisha nasi unaweza kuokoa gharama za hifadhi.

Biashara yetu ya uchapishaji inakupa ubora wa kipekee. Maudhui mazuri yanahitaji kuonekana vizuri: ndivyo tunavyofanya. Magazeti yetu ni maridadi, na huwafanya watangazaji wetu waangaze. Wateja wao wanathamini hilo, na kwa upande wao hutumia katika biashara hiyo. Tunaunda thamani kwao.

Sisi ni mahiri, wenye ufanisi, na wa kutegemewa. Kwa kuwezesha biashara yako na maisha yako, tunaliwezesha taifa.

Vespery Michael

Meneja Uzalishaji na Courier, MCL

LinkedIn: Vespery Michael