Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shalulile amuinua GSM jukwaani

Muktasari:

  • GSM aliyekuwa ameketi katika jukwaa la VIP pamoja na Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said, wote waliinuka wakati Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe, alipomtambulisha rasmi Shalulile mbele ya mashabiki.

Utambulisho wa mshambuliaji mpya wa Yanga, Peter Shalulile, umeibua shangwe kubwa katika kilele cha Yanga Day kinachofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, huku mdhamini mkuu wa klabu hiyo, Ghalib Said Mohamed ‘GSM’, akiinuka jukwaani kwa mshangao.

GSM aliyekuwa ameketi katika jukwaa la VIP pamoja na Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said, wote waliinuka wakati Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe, alipomtambulisha rasmi Shalulile mbele ya mashabiki.

Ujio wa Shalulile umeongeza hamasa kubwa kwenye tamasha hilo kutokana na rekodi yake ya kuvutia akiwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, ambako alikuwa miongoni mwa washambuliaji hatari zaidi katika Ligi Kuu ya nchi hiyo na michuano ya kimataifa.

Shalulile alijiunga na Sundowns mwaka 2020 akitokea Highlands Park na kwa muda wote aliokuwa klabuni hapo alikuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya timu hiyo, akifunga zaidi ya mabao 100 na kusaidia kutwaa mataji mbalimbali.

Akiwa Sundowns, Shalulile alishinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL) mara tano mfululizo, huku akitwaa tuzo ya Mfungaji Bora wa ligi mara tatu mfululizo katika misimu ya 2020/21, 2021/22 na 2022/23.

Pia alitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa PSL msimu wa 2020/21, Players' Player of the Year mara mbili na kumaliza akiwa Mfungaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2023.

Katika kipindi chake Sundowns, Shalulile alifikisha mabao 129 katika PSL, rekodi iliyomweka miongoni mwa wafungaji bora katika historia ya ligi hiyo.

Sasa, ujio wake Yanga umeongeza matarajio makubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo, ambao wanamtazamia kuendeleza makali yake ya kufunga mabao katika soka la Tanzania na michuano ya kimataifa.