Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diarra, Bacca, Yao, Mwamyeto waoengeza mikataba Yanga

Muktasari:

  • Taarifa hiyo ilitolewa na Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, wakati wa kuwatambulisha wachezaji hao mbele ya mashabiki katika hafla ya uzinduzi wa kikosi cha msimu wa 2026/27, maarufu kama Yanga Day.

YANGA imewaongezea mikataba ya miaka miwili nyota wake wanne, Djigui Diarra, Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto na Yao Kouassi, ikiwa ni sehemu ya mipango ya kukijenga kikosi imara kwa ajili ya msimu ujao.

Taarifa hiyo ilitolewa na Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, wakati wa kuwatambulisha wachezaji hao mbele ya mashabiki katika hafla ya uzinduzi wa kikosi cha msimu wa 2026/27, maarufu kama Yanga Day.

Wachezaji hao ni miongoni mwa nyota waliotambulishwa katika hafla hiyo, huku klabu ikionyesha imani yake kwao kwa kuwaongezea mikataba na kuendelea kuwategemea katika mipango yake ya msimu ujao.

Kwa mujibu wa maelezo ya klabu, Diarra na Yao tayari walikuwa wamebakiwa na mwaka mmoja katika mikataba yao, hivyo baada ya kuongezewa miaka miwili, kandarasi zao mpya zitawafikisha hadi msimu wa 2028/29.

Kwa upande wa Bacca na Mwamnyeto, mikataba yao mipya ya miaka miwili inaanza msimu huu wa 2026/27 na itamalizika mwishoni mwa msimu wa 2027/28.

Hatua hiyo imekuja wakati Yanga ikiendelea kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya mashindano ya ndani na ya kimataifa, ikiwa na lengo la kuendelea kuwa miongoni mwa timu zenye ushindani mkubwa barani Afrika.

Taarifa hiyo ilipokelewa kwa shangwe na mashabiki wa Yanga wakati wachezaji hao walipotambulishwa, ishara ya kuonyesha kuwa bado wana imani kubwa na nyota hao kuelekea msimu mpya.