Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TMA FC katika njia ya Ruvu Shooting

TMA Pict

Muktasari:

  • Ruvu Shooting iliyoshuka daraja kutoka Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2022-2023, baada ya kumaliza mkiani mwa nafasi ya 16 na pointi 20, ilipohamia Iringa ikitokea Mlandizi, Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, mambo yalikuwa ni magumu na kupotea.

MWENENDO mbaya wa TMA FC ya Iringa katika Ligi ya Championship msimu huu wa 2026-2027, huenda ukafuata njia ya Klabu ya Ruvu Shooting iliyoweka kambi mkoani humo tangu, Agosti 2023, baada ya kupitia kipindi kigumu chenye misukosuko mingi.

Ruvu Shooting iliyoshuka daraja kutoka Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2022-2023, baada ya kumaliza mkiani mwa nafasi ya 16 na pointi 20, ilipohamia Iringa ikitokea Mlandizi, Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, mambo yalikuwa ni magumu na kupotea.

Baada ya kuhamia Iringa, Ruvu Shooting ilikumbwa na ukata mkubwa wa kifedha wakati ikiwa inashiriki First League msimu wa 2024-2025, jambo lililochangia kuiandikia barua Bodi ya Ligi (TPLB) ya kujitoa na kufungiwa kushiriki misimu miwili.

Hali hiyo ya Ruvu Shooting, inatia shaka pia na ushiriki wa TMA FC katika Ligi ya Championship msimu huu, ambapo tangu imehamia mjini, Iringa ikitokea jijini, Arusha, imekuwa na mwenendo usioridhisha, jambo linaloongeza wasiwasi kikosini.

Tayari TMA FC imekumbwa na rungu la kupokwa pointi tatu na mabao matatu na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB), baada ya timu hiyo kushindwa kusafiri kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, kucheza dhidi ya Stand United 'Chama la Wana', Septemba 25, 2026.

Katika mechi 11, ilizocheza TMA FC hadi sasa, imekusanya pointi tatu tu ikiwa mkiani mwa nafasi ya 16 na mara ya mwisho Ruvu Shooting ikishiriki Ligi ya Championship msimu wa 2023-2024, ilimaliza pia nafasi ya 16, ikiwa na pointi 13.