Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tegisi atikisa Kagame, apewa chapuo la kiatu cha dhahabu

Muktasari:

  • Tegisi, aliyesajiliwa kutoka Pamba Jiji, alifunga mabao mawili katika ushindi wa Singida Black Stars wa 4-1 dhidi ya Mogadishu City kwenye Uwanja wa Kigali Pele, Rwanda, matokeo yaliyoiweka tena kwenye mbio za kutetea taji la michuano hiyo.

MSHAMBULIAJI mpya wa Singida Black Stars, Mathew Tegisi, ameanza kuwa gumzo katika Kombe la CECAFA Kagame baada ya kuonyesha makali yake katika mchezo wa pili wa Kundi B dhidi ya Mogadishu City huku akipigiwa chapuo la kuwania tuzo ya mfungaji bora wa michuano hiyo.

Tegisi, aliyesajiliwa kutoka Pamba Jiji, alifunga mabao mawili katika ushindi wa Singida Black Stars wa 4-1 dhidi ya Mogadishu City kwenye Uwanja wa Kigali Pele, Rwanda, matokeo yaliyoiweka tena kwenye mbio za kutetea taji la michuano hiyo.

Uwezo huo umemfanya kocha Mtanzania Baraka Hussein ambaye amewahi kuinoa Rutsiro FC ya Rwanda, kumpa nafasi mshambuliaji huyo katika vita ya kuwania kiatu cha ufungaji kutokana na kile alichokionyesha ndani ya uwanja.

“Tegisi ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa, kile alichokifanya kwenye mchezo dhidi ya Mogadishu kinaonyesha ana sifa za kuwa mmoja wa wafungaji bora wa mashindano haya, ana kasi, anajua kukaa kwenye nafasi sahihi na ana utulivu anapopata nafasi,” alisema Hussein. Katika mchezo huo, Singida Black Stars ilianza kwa kushtukizwa baada ya Naby Bangoura kuifungia Mogadishu City bao la kwanza dakika ya 10 lakini mabingwa hao watetezi walirejea kwa nguvu na kusawazisha dakika tatu baadaye kupitia Henry David.

Tegisi aliiweka Singida mbele dakika ya 16 kabla ya Henry David kuongeza bao la tatu dakika ya 44 na kuwafanya waende mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 3-1. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi hiyo hiyo, huku Tegisi akifunga bao lake la pili dakika ya 53 na kukamilisha ushindi mnono wa mabao 4-1.

Ushindi huo ulionyesha nguvu ya usajili mpya wa Singida Black Stars.