Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba Day ni Lupopo au Tusker

Muktasari:

  • Taarifa ambazo Mwanaspoti limezipata, zinaeleza kuwa, viongozi wa pande hizo mbili wamekuwa kwenye mazungumzo kwa siku kadhaa na kwa sasa yamefikia hatua nzuri, huku makubaliano yakikaribia kukamilika ili Lupopo iwe mpinzani wa Simba kwenye tamasha hilo litakalofanyika Agosti 8, 2026.

FC Lupopo kutoka DR Congo, inatarajiwa kutua nchini Tanzania kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa mashindano 2026-2027, huku ikitajwa kuwa kwenye mazungumzo ya mwisho ya kucheza na Simba katika mechi ya Simba Day.

Taarifa ambazo Mwanaspoti limezipata, zinaeleza kuwa, viongozi wa pande hizo mbili wamekuwa kwenye mazungumzo kwa siku kadhaa na kwa sasa yamefikia hatua nzuri, huku makubaliano yakikaribia kukamilika ili Lupopo iwe mpinzani wa Simba kwenye tamasha hilo litakalofanyika Agosti 8, 2026.

FC Lupopo ni moja ya klabu kongwe nchini DR Congo ikiwa na historia ndefu katika Ligi Kuu ya nchi hiyo na mara kadhaa imewakilisha taifa hilo katika mashindano ya CAF.

Timu hiyo imekuwa ikisifika kwa soka la kasi na ushindani mkubwa, jambo linalotarajiwa kuongeza mvuto wa tamasha hilo.

Kwa upande wa Simba taarifa za ndani zilisema, maandalizi ya msimu mpya yanaendelea kwa kasi baada ya kufanya maboresho kadhaa ya kikosi, huku benchi la ufundi likihitaji mechi ngumu za kirafiki zitakazowapa wachezaji nafasi ya kujipima kabla ya kuanza kwa mashindano rasmi.

Katika miaka ya hivi karibuni, Simba imekuwa na utamaduni wa kucheza mechi za Simba Day dhidi ya timu zenye hadhi kiwango kikubwa ili kuongeza ushindani na kuwapa mashabiki burudani kabla ya pazia la msimu mpya kufunguliwa.

Wakati huo huo, taarifa kutoka Kenya, zilisema kuwa Simba pia ina uwezekano wa kucheza dhidi ya Tusker FC ya Kenya kwenye Simba Day, lakini hadi sasa mazungumzo na FC Lupopo ndiyo yanayoonekana kuwa na kasi kubwa zaidi na yanakaribia kufikia makubaliano ya mwisho.

Endapo mchakato huo utakamilika, mashabiki wa Simba watapata fursa ya kushuhudia kipimo kizito dhidi ya moja ya timu zenye uzoefu mkubwa kutoka DR Congo kabla ya timu hiyo kuanza safari ya kuwania ushindi katika mashindano ya ndani na kimataifa msimu ujao.