Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TBT ZILITREND: Simba 'yairoga' Yanga

KAMA kawaida tunaendelea kuwakumbushia stori zilizotrendi miaka ya nyuma na jana ikiwa ni Juni 2 tunarudi hadi mwaka 2004 na kukutana na habari iliyobamba kipindi hicho inayohusu Yanga kubwana mbavu katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Ipo hivi. Yanga kipindi hicho ilibanwa mbavu baada ya kukubali kichapo cha kwanza kutoka kwa AFC Arusha, katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Highbury bao pekee la dakika ya 39 lililofungwa na David Mwantope kwa shuti kali lililomshinda kipa, Noel Pompii.
Arusha ilipata bao hilo ikiwa ni dakika tano tu tangu timu ya Simba iingie Uwanjani kwa basi na kuzunguka uwanja mzima huku wachezaji wake wakionyesha vidole viwili kuashirikia timu hiyo ingeshinda mabao mawili.



Baada ya wachezaji wa Simba kushuka kwenye basi lao na kwenda kukaa jukwaani, AFC ilipata bao ambalo lilishangiliwa sana na mashabiki wa Simba ambapo wakati huo ilicheza na Pamba katika mchezo wa kirafiki.
Mwantobe alifunga bao hilo dakika ya 56 baada ya kugongeana pasi na Chesco Mathew lakini mwamuzi Frederick Tibaijuka alikataa kwa madai alikuwa ameotea.
Baada ya mchezo huo wachezaji wa Simba waliokuwa kwenye basi namba TZS 9687 walibaki uwanjani hapo wakiwa na mashabiki zao wakishangilia ushindi wa AFC.
Licha ya kufungwa kipindi hicho ila Yanga iliendelea kuongoza kundi A na pointi zake 24 sawa na Prisons inayoshika nafasi ya pili lakini ina mabao machache ambayo kwa kipindi hicho ilicheza na Mjini Dodoma.