Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yapanda nafasi mbili viwango vya Fifa

 Tanzania imepanda kwa nafasi mbili katika orodha ya hivi punde zaidi ya viwango vya FIFA Duniani, sasa inashika nafasi ya 119, kwa kujikusanyia pointi 1,160.98.

Kupanda huku kumechangiwa na matokeo ya hivi karibuni ya Taifa Stars katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2023) zilizofanyika Abidjan, Ivory Coast, ambapo Tanzania ilishika nafasi ya nne Kundi F, kwa kujikusanyia pointi mbili.
Tanzania ilicheza mechi tatu za fainali za Afcon, ikifungwa mabao 3-0 dhidi ya Morocco, ikitoka sare ya 1-1 dhidi ya Zambia sare tasa dhidi ya DR Congo.

Mechi hizo ndizo pekee zilizozingatiwa kati ya kiwango cha mwisho cha Januari na cha sasa.

Argentina inaongoza kwa pointi 1,855.2, ikifuatiwa na Ufaransa yenye pointi 1,845.44, na Uingereza katika nafasi ya tatu kwa pointi 1,800.05. Ubelgiji inashikilia nafasi ya nne kwa pointi 1,798.46, na Brazil inashika nafasi ya tano kwa pointi 1,784.09.

Barani Afrika, Morocco inashikilia nafasi ya kwanza kwa pointi 1,665.99, ikifuatiwa na Senegal katika nafasi ya pili kwa pointi 1,260.74.

Nigeria inashika nafasi ya tatu kwa pointi 1,522.26, huku Misri ikishikilia nafasi ya nne kwa pointi 1,500.38. Washindi wa Afcon, Ivory Coast, ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 1,494.57, wakipanda nafasi 10 kutoka nafasi yao ya awali ya 49.

Katika ukanda wa Cecafa, Uganda inaongoza kwa pointi 1,246.88, ikishika nafasi ya 92 katika orodha hiyo. Kenya inashika nafasi ya 111 kwa pointi 1,181.92, na Tanzania inashika nafasi ya tatu kwa pointi 1,160.98.

Sudan inashikilia nafasi ya 127 ikiwa na pointi 1,128.74, wakati Rwanda iko nafasi ya 133 (pointi 1,107.04), na Burundi inashika nafasi ya 140 (pointi 1,085.83). Ethiopia iko katika nafasi ya 145 kwa pointi 1,068.79, Sudan Kusini katika nafasi ya 166 kwa pointi 989.29, Djibouti nafasi ya 192 kwa pointi 882.76, na Somalia katika nafasi ya 198 kwa pointi 845.66.