Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF yaishika Yanga pabaya

PABAYA Pict

Muktasari:

  • Karia amezungumza hayo leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari za Michezo katika Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), lililopo Karume, jijini Dar es Salaam.

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema wamerekebisha kanuni ya kuipoka timu pointi tano ikiwa itagundulika imetumia vyumba vya kubadilishia nguo bila sababu za msingi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari za Michezo katika Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema wameandaa vifaa mbalimbali vitakavyotumika katika vyuma vya kubadilishia nguo.

"Kumekuwa na malalamiko mengi ya timu kuhusu vyuma vya kubadilishia nguo, sasa vifaa hivyo tulivyonunua tutavitumia kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa madai mbalimbali ambayo yamekuwa yakisemwa," amesema Karia.

Aidha, Karia amesema ikiwa timu yoyote itatumia vyumba tofauti na vya uwanjani huku uchunguzi ukionekana hakukuwa na shida yoyote, basi timu hiyo itapokwa pointi tano hata kama uwanjani itakuwa imeshinda.

Hatua hiyo inajiri baada ya hivi karibuni Yanga kutozwa kiasi cha Sh100 milioni kutokana na kutumia 'Jumba Jeupe' kwenye kwenye mechi kati ya timu hiyo dhidi ya JKT Tanzania na watani zao wa jadi Simba lililopo Mbweni, jijini, Dar es Salaam.

Karia amezungumza hayo leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari za Michezo katika Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), lililopo Karume, jijini Dar es Salaam.