Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania Prisons mguu sawa Championship

PRISONS Pict

Muktasari:

  • Prisons ambayo ilishuka daraja msimu uliopita kwa play off, msimu ujao itashiriki Ligi ya Championship ikianzia ugenini michezo miwili dhidi ya Rhino Rangers na Mbeya Kwanza, kisha kurejea jijini Mbeya kuikabili Mbuni FC.

WAKATI Ligi ya Championship ikitarajia kuanza Septemba 11, 2026, Tanzania Prisons imesema ipo tayari kuianza upya safari ya matumaini ya kuisaka tena Ligi Kuu, huku ikichekelea ratiba ya kuanzia mechi mbili ugenini.

Prisons ambayo ilishuka daraja msimu uliopita kwa play off, msimu ujao itashiriki Ligi ya Championship ikianzia ugenini michezo miwili dhidi ya Rhino Rangers na Mbeya Kwanza, kisha kurejea jijini Mbeya kuikabili Mbuni FC.

Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Shadrack Nsajigwa amesema maandalizi waliyonayo kwa sasa ikiwamo mechi za kirafiki, yanawapa nguvu na matumaini ya kufanya vizuri msimu huu.

Amesema kuanzia ugenini mechi mbili mfululizo si tatizo kwao kwani maandalizi, nia na utayari wao ndiyo silaha kubwa katika kuvuna pointi tatu kila mchezo, akisifia ubora wa kikosi chake kufanya kweli.

“Tunaendelea vyema na maandalizi na vijana wanaonesha utayari na nia ya kufanya vizuri, maandalizi yetu ndio yatatupa matokeo kwakuwa tumekuwa na muda wa kujiandaa.

“Kwa wiki moja iliyobaki tunaendelea kuboresha timu na kusahihisha makosa lakini kutengeneza muunganiko, kusuka sehemu ya ushambuliaji na beki kuhakikisha tunapoanza ligi tuwe imara,” amesema Nsajigwa.

Kocha huyo mwenye uzoefu wa soka la ushindani, hakusita kutoa tahadhari kwa nyota wake na timu wanazoanza nazo msimu zinao uwezo na uzoefu, hivyo lazima kuwa makini ili kufikia malengo.