Straika la mabao lasaka rekodi
Muktasari:
- Nyota huyo aliyejiunga na Mbeya City msimu huu wa 2026-2027, akitokea Tanzania Prisons ambayo imeshuka daraja hadi Ligi ya Championship, amekuwa mhimili mkubwa kwa timu hiyo kutokana na ki-wango chake.
MSHAMBULIAJI wa Mbeya City, Oscar Mwajanga amesema licha ya kiwango bora anachoendelea kukionyesha na kikosi hicho hadi sasa, ila moja ya malengo yake ni kuhakikisha anaivuka rekodi yake ya mabao ya Ligi Kuu aliyoweka ya msimu wa 2025-2026.
Nyota huyo aliyejiunga na Mbeya City msimu huu wa 2026-2027, akitokea Tanzania Prisons ambayo imeshuka daraja hadi Ligi ya Championship, amekuwa mhimili mkubwa kwa timu hiyo kutokana na ki-wango chake.
Akizungumza na Mwanaspoti, Mwajanga alisema mshambuliaji mzuri anapimwa kwa idadi ya mabao aliyoyafunga na yeye anataka kuonyesha hilo, licha ya kukiri kuna ushindani mkubwa uliopo kutoka kwa nyota wenzake wanaocheza nafasi moja uwanjani.
“Licha ya ushindani ila nitaendelea kuonyesha kipaji changu kadri nitakavyopata nafasi ya kucheza, jambo nzuri tayari nimeshaanza kwa dakika ninazopewa, lengo ni kufanya vizuri na kuepuka presha kama ya msimu uliopita,” alisema Mwajanga.
Aidha, Mwajanga alisema licha ya kutopata nafasi ya kuanza zaidi kikosi cha kwanza, ila kwake halimuumizi kwani anaendelea kumshawishi kocha kumwamini kwa dakika anazompa, kutokana na kile anachoendelea kukionyesha akiwa uwanjani.
“Kila mchezaji ana nafasi ya kucheza kutokana na mahitaji ya timu, ninachokifanya ni kutoa kile kili-chokuwa bora bila ya kujali nimeanza kikosi cha kwanza au nimetokea benchi, kwani lengo letu ni kui-pambania Mbeya City kwa pamoja,” alisema.
Tangu ajiunge na Mbeya City msimu huu wa 2026-2027, akitokea Prisons, tayari amehusika katika mabao manne ya timu hiyo katika Ligi Kuu Bara, baada ya mshambuliaji huyo kufunga matatu na kuasisti moja, akiwa ndiye anayeongoza kikosini humo.