Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanesco yainyuka Polisi 2-0

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoa wa Geita leo Januari 23, 2020 liliandaa Bonanza lililofanyika katika viwanja wa Kharumwa ambalo limejumuisha michezo mbalimbali.

Katika mchezo wa mpira wa miguu Polisi Nyang'wale wameibuka washindi dhidi ya Tanesco Nyang'hwale kwa mabao 2-0.

Michezo mingine iliyofanyika ni kukimbia kuku na kuvutia kamba.

Akifungua bonanza hilo Mkuu wa Wilaya Nyang'wale, Wilson Shimo ameipongeza Tanesco kwa kuandaa bonanza hilo ambapo amesema litaleta umoja baina ya wafanyakazi.

"Niwapongeze washiriki wote wa bonanza, nitoe rai mabonanza haya yasiishie leo, tufanye mara kwa mara kwa ajili ya afya zetu" amesema Shimo.

Kwa upande wake Meneja wa Tanesco Wilaya ya Nyang'wale, Lucas Kalori amesema wataendelea na utaratibu wa kuandaa mabonanza kama hayo.