Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tamko la Polisi kuelekea derby ya Simba v Yanga

Polisi watoa tamko kuelekea derby ya Simba v Yanga

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limejipanga kikamilifu kuhakikisha ulinzi unaimarishwa kwa kiwango cha hali ya juu katika mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga siku ya tarehe 11/12/2021 majira ya saa kumi na moja jioni katika Uwanja wa Benjamini Mkapa lengo ni kuwafanya mashabiki wa mpira wa miguu watakaoshuhudia mchezo huo wawe kwenye mazingira ya Amani na Utulivu.

Jeshi la Polisi kanda Maalumu ya Dar es salaam halitatoa fursa kwa mtu/watu wenye lengo la kufanya vurugu katika mchezo huo na kuharibu miundo mbinu ya uwanja kwa sababu yeyote ile.

 Pia Jeshi linapiga marufuku kwa mtu yeyote yule asiyehusika na mambo ya kiusalama kuingia uwanjai na silaha yoyote ikiwa ni pamoja na silaha za moto, visu, Panga au mawe kwa kufanya hivyo hatua kali zitachukuliwa.

Simba na Yanga zitakutana kesho kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam na mshindi wa mechi hiyo ndiye ataongoza kwenye msimamo ambao sasa Yanga ndio kinara ikiwa na pointi 19 na Simba ni ya pili na pointi 17.