Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sven: Muhimu pointi tatu

USHINDI wa bao 1-0, ambao walioupata Simba dhidi ya KMC jana Desemba 16 umemuibua Kocha, Sven Vandenbroeck na kusema kuwa wana hana wasiwasi wala kujali aina ya bao ambalo limepatikana katika mchezo huo ambao ulikuwa mgumu kwa timu zote mbili.

Sven anasema mechi ngumu na zenye ushindani wa namna ya KMC lazima kutakuwa na matukio kama hayo lakini kwake wala hajali kwa kuwa tayari wameshapata ushindi na pointi tatu ambazo walikuwa hakihitaji katika mchezo huo.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

"Wala siangalii maneno na vitu ambavyo vinazungumzwa huko nje kuwa tumepata ushindi wa bao 1-0 na mambo mengine kubwa tumefanikiwa kupata pointi tatu ambazo tulikuwa tunahitaji na si kitu kingine zaidi ya hapo," anasema.

"Niseme ukweli tangu nimeanza kufundisha soka hapa nchini miongoni mwa timu ngumu ambayo inacheza katika nidhamu na mbinu ni KMC niwapongeze kwa hilo ndio maana mara zote tukikutana nao mechi yetu inakuwa ngumu,” amesema Sven

"Niwapongeze wachezaji wangu kwa ambavyo wamecheza mechi ya Mbeya City muda mfupi ambao tulipata kujiandaa wamefanya kazi kubwa ambayo nilikuwa nahitaji kutoka kwao na walifanyia kazi maelekezo yangu kama ambavyo nilitaka ndio maana nimewapa mapumziko ya siku mbili," amesema Sven

"Mara nyingi mechi za kibingwa au timu zenye sifa ya kuchukua ubingwa lazima ipate matokeo katika mazingira magumu kama ilivyokuwa kwa upande wetu tulivyocheza mechi mbili zilizopita dhidi ya Mbeya City na KMC," amesema Sven.