Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaachiwa msala wa Morrison

SIKU chache baada ya kuzagaa kwa video inayomuonyesha winga wa Simba, Bernard Morrison ‘BM3’ akionyesha ishara ya tusi, imewaibua mabosi wa Bodi ya Ligi (TPLB) na kuwaachia Wekundu wa Msimbazi msala wa Mghana huyo wakidai wao ndio wanaopaswa kumshughulikia kwanza.

Mpaka sasa sio viongozi wa Simba wala wasimamizi wa soka waliozungumzia suala hilo ambalo miaka michache iliyopita liliwahi kumponza nyota wa zamani wa Simba, Yanga na Taifa Stars, Athuman Idd ‘Chuji’ alipowaonyesha mashabiki kidole cha kati walipokuwa wakimzomea.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB), Steven Mnguto alipoulizwa kulikoni juu ya ukimya kuhusiana na video na kitendo alichofanya winga huyo wa zamani wa Yanga, alisema kinapaswa kwanza kuchukuliwa hatua na viongozi wa timu yake kisha liende TFF.

Mnguto alisema hadi sasa hajaona wala kusikia hatua zozote zilizochukuliwa na Simba dhidi ya mchezaji huyo, lakini akadokeza kwa upande wao kama litafika mezani kwao watalipeleka katika kamati ya nidhamu ambayo ndio ina mamlaka ya kutoa uamuzi.

Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Masoko ya TFF, Boniface Wambura alisema hajaliona tukio la mchezaji huyo, ila kabla ya kwenda kwao viongozi wa Simba ndio walitakiwa kuwa wa kwanza kuliongelea au kulitolea tamko.

Hakuna kiongozi wa Simba aliyepatikana kuzungumzia video hiyo ambayo Morrison akiwa ndani ya uzi wa timu yake alitoa ujumbe na kumalizia kwa kuonyesha dole la kati. Kanuni zinakataza wachezaji kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu wakiwa ndani na nje ya uwanja.