Rekodi za ugenini zamtesa Ibenge
Muktasari:
- Katika mechi nne ilizocheza kikosi hicho, mbili imezicheza nyumbani na kushinda zote, ikishinda mabao 2-1, dhidi ya TRA United na 2-1, mbele ya Pamba Jiji, huku ugenini ikitoka sare ya bao 1-1 na Polisi Tan-zania, kisha 2-2 na Geita Gold.
REKODI ya mechi za ugenini za Ligi Kuu Bara kwa Azam FC, zimeendelea kuitesa timu hiyo msimu huu wa 2026-2027, baada ya kutoka sare mbili ilizocheza hadi sasa, ikiwa ni mwenendo usioridhisha kwa kikosi hicho cha Kocha Mkuu, Florent Ibenge.
Katika mechi nne ilizocheza kikosi hicho, mbili imezicheza nyumbani na kushinda zote, ikishinda mabao 2-1, dhidi ya TRA United na 2-1, mbele ya Pamba Jiji, huku ugenini ikitoka sare ya bao 1-1 na Polisi Tan-zania, kisha 2-2 na Geita Gold.
Msimu wa 2025-2026, licha ya Azam FC kumaliza nafasi ya tatu na pointi 64, ila ndio timu iliyoteseka na mechi za ugenini kwani ilitoa sare nyingi tofauti na wapinzani wao Simba waliyomaliza nafasi ya pili na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga.
Katika mechi 15 za ugenini kwa msimu wa 2025-2026, Azam FC ilishinda saba, ikatoa sare sita na kupoteza pia mbili, huku ikifunga mabao 21 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 12 na kikosi hicho kiujumla kilikusanya pointi 27.
Kwa upande wa Simba iliyomaliza nafasi ya pili na pointi 73, katika mechi 15 za ugenini msimu wa 2025-2026, ilishinda 10 na kutoka sare tano na kukusanya jumla ya pointi zake 35, huku kikosi hicho pia kiki-funga mabao 24 na kuruhusu matano.
Kwa Yanga iliyotwaa ubingwa na pointi 73, katika mechi 15 za ugenini kwa msimu wa 2025-2026, ilishin-da tisa, ikatoa sare tano na kupoteza moja na kupata pointi 32, huku safu yake ya ushambuliaji ikifunga jumla ya mabao 22 na kuruhusu sita.
Msimu wa 2026-2027, katika mechi moja iliyocheza Yanga imeshinda mabao matatu na kuruhusu moja, huku kwa upande wa Simba iliyocheza tatu hadi sasa tayari imeshashinda zote na kupata pointi tisa, huku ikifunga mabao sita na kuruhusu mawili.
Kwa maana yake, Azam FC inayosaka taji la Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza tangu ilipochukua kwa mara ya mwisho msimu wa 2013-2014, ina kibarua cha kuchanga vizuri karata zake hususani kwa mechi za ugenini, ili kushindana na Simba na Yanga.
Akizungumzia hilo, Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge alisema wanahitaji kubadilika haraka ili kuendana na ushindani uliopo, huku akiwataka wachezaji wa kikosi hicho kuanza kuonyesha mabadili-ko hayo kuanzia mechi ijayo na Kagera Sugar.
“Mechi yetu ya Agosti 31, 2026, ni lazima tuonyeshe kiwango kikubwa na cha kuvutia ili kupata mato-keo mazuri, haitokuwa rahisi kutokana na mahitaji ya wapinzani wetu pia, ila ni muhimu sana kwetu kupata kilichokuwa bora,” alisema Ibenge.