Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Mtibwa Sugar atangaza vita mpya

MTIBWA Pict

Muktasari:

  • Licha ya kutamani kuibuka mfungaji bora, ila Raizin mwenye bao moja hadi sasa, anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa washambuliaji wengine, wakiongozwa na Hamdan Sarhani wa maafande wa Transit Camp anayeongoza baada ya kufunga mabao 12.

MSHAMBULIAJI wa Mtibwa Sugar, Raizin Hafidh amesema licha ya kasi kubwa inayoendelea kuonyeshwa na washambuliaji wengine wa timu nyingine, ila hajakata tamaa ya kuendelea kupambana, ikiwezekana aibuke mfungaji bora wa msimu huu wa 2026-2027.

Akizungumza na Mwanaspoti, Raizin aliyefunga bao moja hadi sasa, amesema majeraha ya kifundo cha mguu yamechangia kwa kiasi kikubwa kurudisha kasi yake ya kufunga mabao mengi, ingawa, anashukuru kurejea uwanjani kukipigania kikosi hicho.

"Nimekosa mechi sita za Mtibwa Sugar msimu huu kutokana na majeraha yangu ya kifundo cha mguu, hali hiyo imechangia sana mimi kushindwa kufunga zaidi, japo, nashukuru nimerudi salama kwa ajili ya kuendelea kuipigania timu," amesema Raizin.

Nyota huyo aliyewahi kuichezea Dodoma Jiji huku akizichezea pia Gwambina FC na Coastal Union ya Tanga, amesema anawaomba mashabiki waendelee kuwaunga mkono ili wairejeshe Mtibwa Sugar Ligi Kuu, kwa sababu bila wao hawatofikia malengo hayo.

Mshambuliaji huyo anakumbukwa zaidi kwa msimu wa 2024-2025, alipoibuka mfungaji bora wa Ligi ya Championship baada ya kufunga mabao 18, ikiwa ni idadi sawa na Andrew Simchimba aliyekuwa Geita Gold na Abdulaziz Shahame 'Haaland' wa TMA FC.

Licha ya kutamani kuibuka mfungaji bora, ila Raizin mwenye bao moja hadi sasa, anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa washambuliaji wengine, wakiongozwa na Hamdan Sarhani wa maafande wa Transit Camp anayeongoza baada ya kufunga mabao 12.