Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Macha kuifumua Kilimanjaro Wonders

MACHA Pict

Muktasari:

  • Kilimanjaro Wonders ni miongoni mwa timu zilizopanda daraja na kushiriki Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania msimu huu wa 2026/27, lakini mwanzo wake umekuwa mgumu, huku matokeo ya mechi zake za awali yakionyesha kazi kubwa inayomkabili Macha ili kukijenga upya kikosi hicho na kukifanya kiendane na ushindani wa ligi.

KOCHA wa Kilimanjaro Wonders Queens, Daudi Macha amesema atatumia mapumziko ya wiki mbili ya kalenda ya FIFA kufanya marekebisho katika kikosi chake, akitaja safu ya ulinzi kuwa miongoni mwa maeneo yanayohitaji kufanyiwa kazi kwa haraka.

Kilimanjaro Wonders ni miongoni mwa timu zilizopanda daraja na kushiriki Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania msimu huu wa 2026/27, lakini mwanzo wake umekuwa mgumu, huku matokeo ya mechi zake za awali yakionyesha kazi kubwa inayomkabili Macha ili kukijenga upya kikosi hicho na kukifanya kiendane na ushindani wa ligi.

Katika mechi nne ilizocheza, Kilimanjaro Wonders ilianza kwa kupoteza mabao 3-0 dhidi ya Simba Queens, kabla ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mashujaa Queens.

Baadaye ilipata pointi moja baada ya suluhu dhidi ya Fountain Gate Princess, kabla ya kukumbana na kipigo kikubwa cha mabao 7-1 kutoka kwa Yanga Princess.

Matokeo hayo yanaonyesha wazi changamoto inayokikabili kikosi hicho, hasa katika safu ya ulinzi ambayo imeruhusu mabao 12 katika michezo hiyo minne, huku yenyewe ikiwa imefunga mabao mawili pekee.

Macha amekuwa akieleza kuwa kikosi chake kina wachezaji wengi vijana ambao bado wanajifunza namna ya kukabiliana na ushindani na presha ya Ligi Kuu, hasa wanapokutana na timu zenye uzoefu mkubwa kama Simba Queens na Yanga Princess.

Mapumziko hayo yanampa nafasi kocha huyo kufanya marekebisho ya kiufundi, kuboresha mshikamano wa safu ya ulinzi na kuwajenga wachezaji wake kisaikolojia ili warejee wakiwa na ushindani zaidi wakati ligi itakapoendelea Desemba 13.