Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KVZ wana jambo lao Ligi Kuu Zanzibar

KVZ Pict

Muktasari:

  • Novemba 14, 2026, timu hizo zilicheza mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Maisara kisiwani Unguja ambapo Yanga ilishinda kwa mabao 3-1 yaliyofungwa na Cheikh Toure (mawili) na Edmund John ambapo Aziz KI alitoa asisti zote, huku KVZ ikiwa ya kwanza kufunga bao kupitia Mudrick Abdi ‘Gonda’.

KIPA wa KVZ, Idrissa Mguya amesema uzoefu walioupata katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga umeongeza ukomavu wa kikosi hicho na kuwa chachu ya kujiandaa vizuri kwa michezo ijayo ya Ligi Kuu Zanzibar.

Novemba 14, 2026, timu hizo zilicheza mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Maisara kisiwani Unguja ambapo Yanga ilishinda kwa mabao 3-1 yaliyofungwa na Cheikh Toure (mawili) na Edmund John ambapo Aziz KI alitoa asisti zote, huku KVZ ikiwa ya kwanza kufunga bao kupitia Mudrick Abdi ‘Gonda’.

Mguya amesema mchezo huo umewasaidia wachezaji kujifunza namna ya kucheza kwa nidhamu, kujenga mashambulizi kwa haraka na kukabiliana na presha ya mechi kubwa bila kupoteza mwelekeo.

Alifafanua kuwa, faida ya mchezo huo imeanza kuonekana katika namna kikosi hicho kinavyomiliki mpira, kubadilishana pasi kwa kasi na kupunguza makosa yasiyo ya lazima katika maeneo muhimu ya uwanja.

“Wachezaji wameongeza kasi ya kubadilishana pasi, kujipanga vyema wanaposhambuliwa na kutumia nafasi chache wanazozipata mbele ya lango la wapinzani,” amesema.

Amesema benchi la ufundi limekuwa likisisitiza changamoto walizokutana nazo katika mchezo huo hazipaswi kubaki kuwa kumbukumbu, bali zitumike kama sehemu ya kujifunza na kuboresha kiwango chao katika mazoezi ya kila siku.

Aidha, amesema wachezaji wameanza kuonyesha hali nzuri ya kujiamini kutokana na kuelewa majukumu yao wanapokutana na wapinzani wanaotumia mifumo tofauti ya uchezaji.

Mguya anaamini uzoefu huo utaifanya KVZ kuwa timu yenye ushindani mkubwa, uwezo wa kustahimili presha na kutoyumba hata inapokuwa nyuma kwa mabao au inapokutana na upinzani mkali, katika michezo ya ugenini.

KVZ inashika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar baada ya kucheza mechi 11, imekusanya pointi 18 zilizotokana na kushinda mechi tano, sare tatu na kupoteza tatu, ikifunga mabao 12 na kuruhusu manne.