Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stars yaendeleza ubabe kwa DR Congo

Dar es Salaam. Nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta, Simon Msuva na mabeki Kelvin Yondani, Abdi Banda wamechangia kwa kiasi kubwa ushindi wa Taifa Stars wa mabao 2-0 dhidi ya DR Congo iliyosheheni nyota wengi wa kimataifa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Umakini wa beki ya kati Yondani na Banda ulitulia na kumzuia washambuliaji wa DR Congo wakiongozwa na Bennick Afobe anayekipiga katika klabu ya Wolves inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England.

Wakati mabeki hao wakifanya kazi hiyo washambuliaji walikuwa na utulivu wa hali ya juu katika kupeleka mashambulizi kwa Congo wakiongozwa na Samatta, Msuva na Kichuya na kufanikiwa kupata mabao mawili ya dakika za mwisho.

Bao la kwanza lilipatikana baada ya Samatta kutoa pasi kwa Msuva aliyempiga Kichuya aliyepiga krosi iliyomaliziwa na mshambuliaji huyo wa Genk kwa kichwa katika dakika ya 74.

Samatta alitegeneza bao la pili lililofungwa na Kichuya katika dakika 86.

Tanzania imeshinda mechi mara tatu, sare moja na kufungwa mechi mbili mara ya mwisho zilipokutana Februari 23, 2012 timu hizo zilitoka suluhu.