Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arajiga aipeperusha Tanzania CAF

ARAJIGA Pict

Muktasari:

  • Arajiga mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ni miongoni mwa waamuzi 35 watakaopata mafunzo mazuri ya kujiandaa na mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.

MWAMUZI wa kati, Ahmed Arajiga ameendelea kuing’arisha Tanzania katika medali za Mpira wa Miguu, baada ya kuteuliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), awe miongoni wa waamuzi 35, watakaoweka kambi ya mafunzo jijini, Cairo, Misri.

Arajiga mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ni miongoni mwa waamuzi 35 watakaopata mafunzo mazuri ya kujiandaa na mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika nchi zenye mwamuzi mmoja mmoja, ni Tanzania aliyoteuliwa Arajiga, Mahamat Allaou (Chad), Omar Artan (Somalia), Sy Issa (Senegal), Uwikunda Samuel (Rwanda), Melki Mehrez (Tunisia), Lucky Kasalirwe (Uganda) na Hillary Hambaba za Zambia.

Wengine ni Daniel Laryea wa Ghana, Chimene Brighton wa Zimbabwe, Pacifique Ndabihawenimana wa Burundi na Jean Jacques Ndala wa DR Congo na kuhitimisha jumla ya waamuzi 12, ambao nchi zao zimetoa mwamuzi mmoja mmoja katika mafunzo hayo.

ARAJ 01

Morocco wameteuliwa wanne, Jayed Jalal na Kech Chaf Mustapha, huku El Fariq Hamza na Zakaria Bouchtaoui wakiwa kwenye VAR, wakati Afrika Kusini ina watatu ambao ni Tom Abongile na Jelly Alfred Chavani, huku Akhona Makalima akisimamia VAR.

Kenya, itakuwa na waamuzi wawili, wakiongozwa na Peter Waweru Kamaku na Dickens Mimisa atakayesimamia VAR, huku Misri ikiwa na Ahmed Nagy Mosa, Maarouf Mohamed, Mohamed Amin, wakati Hagag Hossam na El Ghandour Ahmed watakuwa VAR. 

Mauritania itakuwa na waamuzi watatu, ambao ni Dahane Beida na Bouh Abdelaziz, huku katika VAR akiteuliwa Sarr Babacar, huku Sudan wakiteuliwa wawili ambao ni Ismail Mahmood na Yasir Ahmed Abdalaziz aliyeteuliwa kusimamia upande wa VAR.

ARAJ 02

Algeria wako wanne ambao ni Benbraham Lahlou, Ghorbal Mustapha na Loutfi Bekouassa huku Boukhalfa Nabil akiteuliwa kwa upande wa VAR na kuhitimisha jopo la waamuzi 35, walioteuliwa na CAF kwa ajili ya mafunzo hayo, jijini, Cairo, Misri.

Mafunzo hayo yataanza rasmi Novemba 18 hadi 23, kuwaandaa waamuzi hao kabla ya kuanza kwa mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika 2026-2027.