Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sowah aendeleza moto Ligi Kuu, Kagera Sugar ikibanwa Kaitaba

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera, wenyeji walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 12, kupitia Khasim Fekha aliyemalizia kwa kichwa mpira wa kutenga uliopigwa na nahodha, David Luhende.

MSHAMBULIAJI wa Singida Black Stars, Mghana, Jonathan Sowah, ameendelea kung'ara na kikosi hicho, baada ya leo kuifungia tena bao muhimu katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyomalizika kwa timu hiyo kulazimisha sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Kagera Sugar.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera, wenyeji walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 12, kupitia Khasim Fekha aliyemalizia kwa kichwa mpira wa kutenga uliopigwa na nahodha, David Luhende.

Licha ya Kagera Sugar kwenda hadi mapumziko ikiwa kifua mbele, Singida ilirejea kwa kasi kipindi cha pili na dakika ya 51, mshambuliaji wa timu hiyo, Jonathan Sowah aliifungia bao la kuchomoa akimalizia pasi ya Jeancy Mboma Kinda.

Bao hilo la Sowah linamfanya nyota huyo kuendeleza kiwango bora akiwa na kikosi hicho msimu huu ambapo hadi sasa amefikisha mabao mawili ya Ligi Kuu Bara akiwa ndiye anayeongoza, tangu arejee kikosini humo Julai 15, 2026, akitokea Simba.

Sowah aliyerejea Singida Julai 15, 2026, akitokea Simba aliyoitumikia kwa msimu wa 2025-2026, amefunga bao hilo na kufikisha mawili, baada ya Agosti 14, 2026, kuifungia pia timu hiyo katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate.

Mshambuliaji huyo raia wa Ghana, licha ya kutabiriwa makubwa na kikosi hicho cha Msimbazi kwa msimu wa 2025-2026, ila alishindwa kuwika kutokana na sababu mbalimbali za nje ya uwanja, ambapo alimaliza kwa kufunga mabao matatu ya Ligi Kuu.

Kabla ya kucheza Simba, Sowah aliyejiunga na Singida Black Stars katika dirisha dogo la Januari 2025, akitokea Al-Nasr Benghazi SC ya Libya, aliifungia mabao 13 ya Ligi Kuu Bara kwa takribani miezi sita, jambo lililoivutia Simba kumsajili.

Kwa upande wa Fekha anakuwa ni mchezaji wa kwanza wa Kagera kuifungia bao la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2026-2027, baada ya kikosi hicho kilichopanda daraja kuanza kwa kuchapwa mabao 2-0 dhidi ya Simba, Agosti 16, 2026.

Kagera iliyorejea Ligi Kuu Bara msimu wa 2025-2026 baada ya kushuka daraja na kushiriki Ligi ya Championship kwa msimu wa 2024-2025, imeanza kwa kucheza mechi mbili za mwanzo kwenye Uwanja wa Kaitaba na kupata pointi moja tu kati ya sita.

Kwa upande wa Singida iliyoanza kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate, inafikisha pointi nne katika mechi zake mbili ilizocheza hadi sasa, huku ikishika nafasi ya pili, nyuma ya vinara Simba inayoongoza ikiwa na pointi sita.