Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Soka la mtaani lapigiwa chapuo kukuza vipaji

Muktasari:

  • Programu ya ugawaji wa vifaa vya michezo kwa timu za mpira wa miguu, inayoitwa Kits for Africa katika ngazi ya bara la Afrika ilizinduliwa Machi 2022 ikilenga kusaidia maendeleo ya michezo nchini Tanzania kwa kutoa vifaa kwa timu za soka ngazi ya chini kabisa.

Dar es Salaam. Katika mkakati wa kukuza vipaji hususani katika mchezo wa mpira wa miguu nchini, wito umetolewa kuchangia mchezo huo ili kukuza vipaji.

Hayo yameelezwa jana Desemba 9 na Ofisa Masoko wa kampuni ya Betway Tanzania, Calvin Mhina katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu za mpira wa miguu iliyofanyika Mbagala Zakhiem.

Ameeleza nia ya kampuni hiyo kuendelea kutoa mchango wake katika sekta ya michezo nchini kwa kuendesha programu mbalimbali zenye manufaa kwa wananchi ikiwemo program ya kugawa vifaa vya michezo kwa timu za mtaani.

Mhina alisisitiza kwamba mwendelezo wa pgoramu hii pia umetokana na mrejesho mzuri uliotolewa na wadau wakati na baada ya uzinduzi uliofanyika Tegeta, Dar es Salaam mwaka jana.

“Leo tuko hapa Mbagala na tunafuraha kuona wanamichezo na wakazi wa Mbagala wanafurahia kupata vifaa hivi kama ambavyo wanamichezo wa Tegeta walifurahia wakati tunazindua program hii mwaka jana,” amesema Mhina.

Hadi Novemba mwaka huu, Betway iligawa vifaa na kuendesha mashindano ya Kombe la Mbuzi yaliyoshirikisha timu nne za Mbagala Zakhiem wilaya ya Temeke, jijini Dare es Salaam.

Timu zilizopata vifaa hivyo na kuingia katika michuano ya Kombe la Mbuzi ni Mizozo FC, Mnarani FC, Wajuba FC, na Mtoni Boys FC. Wajuba FC waliibuka washindi wa jumla na kupata zawadi ya mbuzi wawili baada ya kuifunga Mtoni Boys kwa 2-1.

Kwa upande wake Ofisa Uendeshaji wa Betway Tanzania, Jimmy Masaoe amebainisha kuwa uamuzi wa kampuni hiyo kuangazia soka la mtaani ni sehemu ya kutoa mchango wake kwa jamii na kuchangia katika kukuza maendeleo ya sekta ya michezo nchini Tanzania.

"Programu hii inaitwa Kits for Africa katika ngazi ya bara la Afrika. Katika programu hii Betway inatoa vifaa kwa timu za mtaani ili kusisimua michezo katika ngazi ya chini kabisa kwani huko ndiko ambako vipaji vinakozaliwa.

“Kwa hapa Tanzania, programu hii pia itakuwa na mchango mkubwa katika kuongeza thamani ya michezo katika ngazi za mitaa.

“Tumeamua kwenda kugawa vifaa katika vibanda vya kuonesha michezo maarufu kama Vibanda umiza na kufanya mashindano ya Kombe la Mbuzi katika viwanja vya mtaani kabisa ili kugusa vipaji vya mtaani moja kwa moja,” amesema Masaoe.

Akizungumzia vifaa hivyo, nahodha wa Wajuba FC iliyopokea vifaa, ameipongeza kampuni hiyo kwa mpango wake huo na kusema kuwa itaamsha ari ya wanamichezo mitaani na kurudisha hamasa ya vijana kushiriki michezo katika ngazi za mitaa.

“Kutokana na uhalisia wa maisha imekuwa vigumu kupata kiasi cha kutosha kununua vifaa vyenye ubora kama vilivyotolewa na Betway na hii imekuwa kikwazo kikubwa kwa wengi wanaopenda michezo kushiriki mashindano.

“Najua hii kwangu binafsi na kwa timu zote zilizopata vifaa siku ya leo itachochea ushiriki wetu kwenye michezo,” amesema.