Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

King Sule awaita vijana kwenye ngumi

BONDIA Pict

Muktasari:

  • King Sule amesisitiza mafanikio hayo yanapaswa kuwa chachu kwa vijana wengine kujitokeza katika mchezo huo, huku akiwataka wazazi na wadau wa michezo kuendelea kuwaunga mkono vijana wenye vipaji ili waweze kufikia ndoto zao.

BONDIA namba moja Zanzibar, Suleiman Juma 'King Sule' amewataka vijana kujiunga na mchezo wa ngumi kwani unajenga nidhamu, afya na kuwapa fursa ya kufikia mafanikio ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, King Sule amesema ngumi zimemfungulia milango ya kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa na kuitangaza Tanzania katika medani ya kimataifa.

Amesema anajivunia kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo, jambo ambalo limethibitisha vijana wa Tanzania wana uwezo wa kufanya vizuri wanapopata maandalizi na msaada unaostahili.

"Mafanikio yanapaswa kuwa mfano kwa vijana wanaotamani kujenga maisha kupitia michezo na nasisitiza nidhamu ya mazoezi ya kujituma na uvumilivu ni msingi wa kufikia mafanikio katika ngumi," amesema

Aliongezea; ni muhimu kwa jamii kubadili mtazamo kuhusu mchezo wa ngumi na kuutambua kama taaluma inayoweza kuzalisha mabingwa, ajira na kuitangaza nchi kimataifa.

Hivyo, amewahimiza vijana kutumia vipaji vyao kwa njia chanya badala ya kujihusisha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha mustakabali wa maisha yao.

King Sule amesisitiza mafanikio hayo yanapaswa kuwa chachu kwa vijana wengine kujitokeza katika mchezo huo, huku akiwataka wazazi na wadau wa michezo kuendelea kuwaunga mkono vijana wenye vipaji ili waweze kufikia ndoto zao.