Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yashusha mtu mpya!

MTU Pict


WAKATI mabingwa watetezi wa Kombe la CRDB, Klabu ya Simba ikienda kusherehekea kilele cha Simba Day, tamasha litakalofanyika Jumamosi Agosti 8, 2026, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, mabosi wa timu hiyo wamemuongeza mtaalamu mwingine mpya.


Mtaalamu huyo aliyeongezwa ni Mtathimini wa Michezo (Performance Analyst), Tshepo Boshielo aliyetokea Sekhukhune United FC ya kwao Afrika Kusini, akija kuongeza nguvu katika benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker.


Hatua ya Simba kumuongeza mtaalamu huyo mpya katika benchi la ufundi, ni baada ya Prinil Deen aliyekuwa anahudumu kwenye nafasi hiyo kuondoka kufuatia msimu wa 2025-2026 kuisha, akihudumu ndani ya kikosi hicho cha Msimbazi kwa miezi saba.

Deen aliondoka ndani ya kikosi hicho baada ya Simba kutwaa ubingwa wa Kombe la CRDB msimu wa 2025-2026, jambo ambalo limewafanya mabosi wa timu hiyo kuingia sokoni kutafuta mbadala wake, ambapo kwa sasa imekamilisha usajili wa Boshielo.

MPY 01
MPY 01

Boshielo ni mtaalamu wa uchambuzi wa utendaji wa wachezaji na timu za mpira wa miguu (Performance Analyst) kutoka Afrika Kusini, akiwa na uzoefu wa matumizi ya takwimu za mechi, baada ya kufanya kazi akiwa na kikosi cha Sekhukhune United FC.

Majukumu yake yanajumuisha kuchambua video za mechi, kutathmini viwango vya utendaji wa wachezaji binafsi na timu kwa ujumla, akiandaa taarifa za kiufundi kwa benchi la ufundi na kufanya uchambuzi wa wapinzani ili kusaidia pia maandalizi.

Kupitia utaalamu wake katika uchambuzi wa data na video za michezo, Boshielo anachangia kuboresha uamuzi wa kiufundi, maendeleo ya wachezaji na utekelezaji wa mbinu za mchezo, huku akiisaidia Simba kufikia malengo yake ya kiushindani.