Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yageukia marathon, ngumi

Muktasari:

  • Simba inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 15 sawa na Yanga inayoongoza kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Simba imeandaa mbio za Marathon siku ya Jumapili, Oktoba 4, 2026 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya klabu hiyo kutimiza miaka 90 mwaka huu.

Meneja habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema mbio hizo zitaenda sambamba na michezo mingine kama ngumi na mpira wa kikapu.

"Kwanini Simba Marathon? sababu ya kwanza ni kuazimisha miaka 90 ya Simba. Tunao mashabiki wa aina mbalimbali, tunao wanaopenda boxing (ngumi) ipo siku tutaandaa Simba Boxing.

“Tunao mashabiki wanapenda kuogelea, tunao mashabiki wanapenda basketball (mpira wa kikapu). Yote hayo ni maadhimisho ya miaka 90, tutamgusa kila mtu, unaipenda Simba lakini una kitu chako kingine unakipenda, tutakugusa.

"Tutakuwa na mbio za 5KM, 10KM na 21KM. Ruti yetu itaanzia hapa hapa fukwe ya Coco. Tutakuja kuwatangazia sehemu ambazo wakimbiaji watapita na tutakuwa. Tutakuwa na zawadi kwa wakimbiaji watatu wa kila mbio. Simba tukifanya jambo letu lazima tufanye tofauti, ubora na ukubwa

Ahmed amesema lengo lingine la kuandaa jambo hilo ni kujiweka karibu zaidi na jamii.

"Tunafanya kutanua wigo wa mashabiki, wasiishie kwenye mpira, waende pia kwenye riadha. Lakini pia kuongeza mashabiki, wapo watu hawapendi mpira lakini wanapenda riadha hivyo atajiunga na Simba kupitia riadha.

“Tulifanya utafiti kwenye riadha kuna watu wanapenda mpira na wengine hawapendi, sasa tunawavuta na hao kuwa Simba. Lakini pia tunataka kuwa karibu na jamii, tunadanya tukio la kuwagusa wanajamii. Tuwaombe Wanasimba kujiunga kwa wingi katika tukio hili la Simba Marathon,” amesema Ahmed Ally.