Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba waonywa kabla ya Dabi, Manqoba awataja wachezaji hatari

Muktasari:

  • Mngqithi amesema licha ya muda mfupi wa maandalizi, kikosi chake kitaingia uwanjani kikiwa na hesabu za kushinda na kuendeleza mafanikio yao.

Kocha wa Yanga, Manqoba Mngqithi, amesema kikosi chake kipo tayari kuipa Simba mtihani mzito katika mchezo wa Ngao ya Jamii, huku akiwataja baadhi ya mastaa wa wapinzani wao hao ambao anawaona kuwa tishio katika mchezo wa kesho.

Mngqithi amesema licha ya muda mfupi wa maandalizi, kikosi chake kitaingia uwanjani kikiwa na hesabu za kushinda na kuendeleza mafanikio yao.

“Hii itakuwa mechi yangu ya kwanza ya dabi. Natamani kuona inakuwaje katika mechi kubwa kama hii. Bahati mbaya timu zote hazijapata muda wa kutosha kujiandaa kwa mchezo huu kutokana na ratiba ya timu zote mbili wikiendi iliyopita,” amesema.

Ameongeza: “Mashabiki wetu wanatamani kuona tunalinda mafanikio yetu, na sisi kama timu tupo tayari kulikamilisha hilo. Tutaingia tukiwa na akili ya kutafuta ushindi ili tuweke sawa hesabu zetu.”


AWATAJA MASTAA WA SIMBA

Mngqithi amewataja wachezaji wa Simba, Ellie Mpanzu, Lebase Gueye, Ibraheem Jabaar na Keletso Makgalwa, akisema anawafahamu na kwamba Yanga inapaswa kuwa makini ili wasipewe nafasi ya kuonyesha ubora wao.

“Nawajua baadhi ya wachezaji wa Simba. Kuna Mpanzu (Ellie), ni mchezaji mzuri, ana kasi na ubunifu. Kuna Gueye (Lebase), anajua kutengeneza madhara. Kuna yule raia wa Nigeria aliyetokea Stellenbosch, Ibraheem Jabaar, ni mchezaji mzuri. Hata Keletso (Makgalwa) ni mchezaji mzuri. Tunatakiwa kuwa makini nao," amesema.

“Hatutaingia kwenye mechi hii kushangaa. Tutakwenda kuwapa maswali magumu Simba. Tuna wachezaji wazuri ambao wanaweza kutupa kitu tunachotaka.”

Beki wa Yanga, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, amesema wachezaji wanafahamu umuhimu wa kupata ushindi katika mchezo huo na wamejipanga kuwafurahisha mashabiki wao.

“Wachezaji tupo tayari kutekeleza yale ambayo makocha wetu wametufundisha. Sisi kama wachezaji tunajua umuhimu wa ushindi kwenye mechi kama hii. Tunataka kushinda, mashabiki wetu waje kwa wingi,” amesema Tshabalala.