Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba Queens waisaka fainali ya Cecafa

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya Klabu Bingwa kwa soka la Wanawake kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Women), Simba Queens leo inarudi tena uwanjani kuvaana na Vihiga Queens katika mchezo wa nusu fainali ya hatua ya awali ya kufuzu fainali za Klabu bingwa Afrika (CAF).

Michuano hiyo ya Afrika itakayofanyika kwa mara ya kwanza itapigwa Cairo, Misri na timu za Cecafa zinaumana jijini Nairobi, Kenya na Simba Queens ilifuzu hatua hiyo baada ya kufanye vema katika mechi za makundi ikiwamo kuwanyoa Wadjibouti kwa mabao 10-0 wikiendi iliyopita.

Simba iliongeza kundi A, leo itavaana na wenyeji wao, Vihiga ya Kenya walimaliza nafasi ya pili katika Kundi B lililoongozwa na CBE ya Ethiopia, ili kusaka fainali. Simba itacheza leo na mshindi kati ya vinara wa Kundi B CBE ya Ethiopia dhidi ya Lady Doves WFC ya Uganda.

Vihiga Queens ni timu ya pili katika michuano hii kufunga mabao mengi katika micheza mitatu waliocheza Vihiga wamefunga mabao 21 wakiruhusu mabao manne kwa upande wa Simba imetupia kambani mara 14 wakifungwa 1 na kwa takwimu hizo Vihiga ni timu ya kuchunga sana.

Simba inapaswa kuwa makini ni nyota wa Vihiga wakiongozwa na Maureen Achieng anayevaa jezi namba 10 akiwa amefunga mabao matano sawa na Jentrix Shikangwa, pia kuna Violet Wanyonyi mwenye mabao manne, huku nyota wa Simba hasa wa ushambuliaji wajipange dhidi ya ukutra mgumu wa wapinzani wao hao chini ya kiungo mkabaji Joan Nabirye.

Kocha Mkuu wa Simba Queens, Hababuu Ali aliliambia Mwanaspoti kuwa, anatambua na mchezo mgumu kwani anaenda kucheza na timu yenye safu ya ushambuliaji nzuri.

“Tunatambua tunakutana na timu ngumu yenye safu nzuri ya ushambuliaji ila tutapambana kutimiza lengo letu la kutwaa ubingwa na kuweza kuwakilisha Cecafa kwenye Klabu Bingwa Afrika kule, Misri”, alisema Hababuu.

Kikosi cha Simba kwenye mchezo wa leo kimeanza na nyota wake kama Joela Bukuru, Aisha Juma, Mawete Musolo, Oppa Clement na wengine kuendeleza moto walioanza nao kwenye hatua ya makundi na kufanya wawe gumzo kwa mashabiki wachache wanaohudhuria mechi hizo kwenye Uwanja wa Moi Kasarani.


IMEANDIKWA NA LILIAN MUKULU