Simba mziki mnene kuivaa Mlandege
Unguja. Kocha wa Simba, Pablo Franco leo Ijumaa ameingiza asilimia kubwa ya nyota wa kikosi cha kwanza kukabiliana na Mlandege FC ikiwa ni mechi ya kuamua nani anatinga nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Tayari timu tatu Yanga, Azam na Namungo zimetinga hatua hiyo ambapo Namungo anamsubiri mshindi kati ya Simba na Mlandege.
Simba walishinda mechi yao ya kwanza hivyo wana pointi tatu wakati Mlandege ana pointi moja baada ya sare ya awali hivyo kama atashinda atakisha pointi nne na Simba akishinda atakuwa na pointi sita na akitoka sare wote watakuwa na pointi sawa, nne hivyo idadi ya mabao ndiyo itakayoamua.
Mechi hiyo inatarajia kuanza saa 2.15 usiku na golini atasimama Aishi Manula, Israel Mwenda, Gadiel Michael, Pascal Wawa, Henock Inonga, Jonas Mkude, Denis Kibu, Mzamiru Yasin, Chris Mugalu, Pape Sakho na Yussuf Mhilu