Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sikia Mgosi anachowaambia mastaa Simba

MGOSI Pict

Muktasari:

  • Mgosi, ambaye ni kocha wa Simba Queens, ameyasema hayo kutokana na uzoefu alionao wa kushiriki matamasha hayo kwa nyakati tofauti. Ni miongoni mwa mastaa walioshiriki tamasha la kwanza la Simba Day mwaka 2009, lililoanzishwa chini ya uongozi wa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Hassan Dalali ‘Field Marshal’.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Mussa Hassan Mgosi, amesema tamasha la Simba Day ni picha halisi inayowaonyesha wachezaji ukubwa wa klabu hiyo na kuwaandaa kutambua imani ya mashabiki pamoja na majukumu makubwa yaliyopo mbele yao katika msimu husika.

Mgosi, ambaye ni kocha wa Simba Queens, ameyasema hayo kutokana na uzoefu alionao wa kushiriki matamasha hayo kwa nyakati tofauti. Ni miongoni mwa mastaa walioshiriki tamasha la kwanza la Simba Day mwaka 2009, lililoanzishwa chini ya uongozi wa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Hassan Dalali ‘Field Marshal’.

“Kitendo cha viongozi kuwatambulisha wachezaji mbele ya mashabiki wanaotoka ndani na nje ya Tanzania, ambao wanatenga bajeti kuhakikisha wanafika kuiona timu yao, kinaonyesha ukubwa wa jukumu walilonalo wachezaji. Mashabiki wanakuwa wamesubiri kuona kikosi chao kitakachowapa furaha, hivyo kazi ya wachezaji inakuwa ni kusubiri kuanza kwa majukumu,” amesema Mgosi na kuongeza:

MGO 01

“Heshima wanayopewa wachezaji siku hiyo inakuwa ni deni kwao kujipanga kwa ajili ya kupigania malengo ya klabu. Ndiyo maana nasema tamasha hilo linatoa picha halisi ya mashabiki kuwakabidhi majukumu wachezaji wa timu wanayoishabikia.”

Nahodha huyo wa zamani wa Simba alisajiliwa kwa mara ya kwanza na klabu hiyo mwaka 2005 na kuitumikia hadi 2011, kabla ya kuondoka na kujiunga na DC Motema Pembe msimu wa 2011/12.

Baadaye alirejea nchini na kuzichezea JKT Ruvu na Mtibwa Sugar, kabla ya kurejea tena Simba na kuitumikia hadi alipostaafu soka Agosti 15, 2016.

MGO 02

“Simba Day inakutambulisha kwa ukubwa. Hivyo, jina lako linapokuwa limetangulia mbele ya mashabiki, mchezaji unatakiwa kujipanga kuhakikisha kiwango chako kinakuwa juu ili kuisaidia timu kufikia malengo yake,” amesema.

Mgosi, ambaye msimu wa 2010/11 alikuwa kinara wa mabao ya Ligi Kuu Bara akiwa amefunga 18, alisema wachezaji wanapaswa kutumia nafasi wanayopewa katika klabu kubwa kama Simba au Yanga kujijengea heshima.

“Ukicheza Simba au Yanga na ukafanya vizuri, unajijengea heshima isiyofutika mbele ya mashabiki. Hivyo, naamini wachezaji wapya ndani ya vikosi hivyo, baada ya matamasha, watapata utulivu wa kujipanga zaidi kwa ajili ya majukumu yaliyopo mbele yao,” amesema mkongwe huyo.

MGO 03

Akaongeza: “Lakini pia kwa timu ya Simba Queens, huwa nawashauri wachezaji kuitumia vizuri siku hiyo ili kutambua heshima kubwa wanayoipata mbele ya mashabiki kwamba inatokana na kazi yao nzuri wanayoifanya.”