Ferran Torres atua psg kwa euro milioni 50
Muktasari:
- Klabu hizo mbili zimethibitisha kukamilika kwa uhamisho huo leo, Agosti 15, 2026, huku Torres akitia saini mkataba utakaomuweka PSG hadi mwaka 2031.
NI rasmi kwamba PSG imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania, Ferran Torres, kutoka Barcelona kwa ada ya Euro 50 milioni.
Klabu hizo mbili zimethibitisha kukamilika kwa uhamisho huo leo, Agosti 15, 2026, huku Torres akitia saini mkataba utakaomuweka PSG hadi mwaka 2031.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 atavaa jezi namba 9, akitarajiwa kuwa sehemu muhimu ya safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao wa Ufaransa na Ulaya.
Torres amekuwa sehemu ya kikosi cha Barcelona, lakini akiwa amebakiza mwaka mmoja pekee kwenye mkataba wake imeamua kumuuza ili kupata manufaa ya kifedha badala ya kumpoteza baadaye bila kupata ada kubwa.
PSG sasa inatarajiwa kumtumia nyota huyo zaidi katika nafasi ya mshambuliaji wa kati, hasa baada ya kuondoka kwa Goncalo Ramos aliyejiunga na AC Milan.