Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Seif iddi akili yake kimataifa

SEIF Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo anayevaa jezi namba 10, mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo wa kati na winga zote mbili, amekuwa miongoni mwa wachezaji wanaotegemewa katika kikosi cha Muembe Makumbi kutokana na kasi, uwezo wa kutengeneza nafasi na kupiga mashuti.

BAADA ya misimu minne ya kupambana katika Ligi Kuu Zanzibar na kufunga mabao 39, kiungo mshambuliaji wa Muembe Makumbi City FC, Seif Iddi Juma, amesema sasa anahitaji changamoto mpya nje ya Tanzania ili kuendeleza kipaji chake na kuonyesha uwezo wake katika medani za kimataifa.

Seif amesema amejifunza mengi kupitia soka la Zanzibar na anaamini muda umefika wa kupiga hatua nyingine kwa kutafuta nafasi ya kucheza ligi kubwa barani Afrika na hata nje ya bara hilo.

Nyota huyo anayevaa jezi namba 10, mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo wa kati na winga zote mbili, amekuwa miongoni mwa wachezaji wanaotegemewa katika kikosi cha Muembe Makumbi kutokana na kasi, uwezo wa kutengeneza nafasi na kupiga mashuti.

Akizungumzia mwenendo wa Muembe Makumbi msimu huu, Seif alikiri kutoridhishwa na matokeo ya mwanzo wa ligi, licha ya kukusanya pointi 18 na kushika nafasi ya sita katika msimamo.

Hata hivyo, amesema bado hawajakata tamaa katika mbio za ubingwa, akiamini kuwa wana nafasi ya kubadilisha hali hiyo endapo wataongeza juhudi na kupata matokeo mazuri katika michezo 19 iliyosalia.

“Bado tuna nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa endapo tutafanya kazi ya ziada, kushinda mechi zijazo na kupunguza pengo la pointi dhidi ya timu zilizo juu yetu,” amesema.

Katika malengo yake binafsi, Seif amesema amejipanga kufunga zaidi ya mabao 10 msimu huu ili kuvunja rekodi yake ya mabao tisa aliyofunga msimu uliopita na kuendelea kujijengea nafasi ya kupata timu nje ya nchi.

Ameongeza kuwa kucheza Ligi Kuu Zanzibar kumemjenga kwa kiasi kikubwa kisoka, tofauti na kipindi alipokuwa akicheza katika madaraja ya chini, akitaja nidhamu, kujituma na kufuata maelekezo ya makocha kuwa miongoni mwa mambo yaliyomsaidia kufikia kiwango alichonacho sasa.

Kwa sasa kiungo huyo ana malengo mawili, kwanza kuisaidia Muembe Makumbi City kupambania ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar, pili kutumia kiwango chake kufungua milango ya kucheza soka nje ya Tanzania.