Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Mafunzo aweka mkakati mpya

MWAMGONDE Pict

Muktasari:

  • Mwamgonde amewataka mashabiki wa Mafunzo kuendelea kukiunga mkono kikosi hicho, akiahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha timu hiyo inawapa furaha kupitia matokeo mazuri.

KOCHA Mkuu wa Mafunzo, Innocent Mwamgonde, amesema timu yake imeondokana na hofu iliyokuwa nayo mwanzoni mwa msimu wa 2026-2027 wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL), akieleza kuwa sasa anaelekeza nguvu katika kuboresha eneo la ushambuliaji ili kuongeza makali ya kikosi hicho.

Mwamgonde amesema kurejea kwa timu katika hali nzuri ya ushindani kumempa nafasi ya kuangalia upya mikakati yake, huku akisisitiza kuwa kazi kubwa iliyopo sasa ni kuhakikisha washambuliaji wanakuwa na ufanisi zaidi katika kutumia nafasi wanazozipata.

Alifafanua kuwa, changamoto kubwa iliyokuwa ikiisumbua Mafunzo mwanzoni mwa msimu ni eneo la ushambuliaji, ambalo kwa sasa wanaendelea kulifanyia marekebisho ili kuongeza ubora wa timu katika kila mchezo.

“Tunahitaji kuliweka sawa eneo hilo kwani washambuliaji ndiyo watu wenye uamuzi katika eneo la umaliziaji,” amesema Mwamgonde.

Kauli ya kocha huyo inakuja wakati Mafunzo ikianza kuonyesha dalili za kuimarika baada ya mwanzo mgumu wa ligi, ambapo sasa imefanikiwa kushinda mechi nne kati ya 13 ilizocheza, huku sare zikiwa nne na kupoteza tano.

Matokeo hayo yameifanya kufikisha pointi 16 na kupanda hadi nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi hiyo, baada ya awali kuwa katika eneo la hatari la kushuka daraja.

Mabadiliko hayo yameanza kurejesha matumaini kwa kikosi hicho, ambacho sasa kinaonekana kupata nafuu ya ushindani huku kikiwa na nafasi ya kuboresha zaidi matokeo yake katika michezo inayofuata.

Mwamgonde amewataka mashabiki wa Mafunzo kuendelea kukiunga mkono kikosi hicho, akiahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha timu hiyo inawapa furaha kupitia matokeo mazuri.