Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sapraizi ya kusikilizia Simba

DALA Pict


Huenda Klabu ya Simba ikawashangaza mashabiki wake leo katika tamasha la Simba Day linalofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, mahali ambapo lilizinduliwa mara ya kwanza mwaka 2009 chini ya uongozi wa mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Hassan Dalali ‘Field Marshal’.


Ipo hivi; baada ya burudani mbalimbali zitakazokuwapo katika tamasha hilo itakapofika wakati wa kutambulisha kikosi cha msimu mpya, kuna uwezekano mkubwa mashabiki wakaona sura mpya ambazo hawakuzitarajia.


Mwanaspoti limepata taarifa za ndani kuhusu uwepo wa mshambuliaji Gelson Dala, mchezaji wa timu ya Taifa ya Angola, ambaye inaelezwa kuwa yupo kambini Simba tangu juzi.

DALAS01

Chanzo cha ndani kimesema kuna uwezekano mkubwa Simba imemsajili Dala kwa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya msimu unaoanza Agosti 14, 2026.

Dala anatarajiwa kusaidiana na Clatous Chama, aliyemaliza msimu uliopita akiwa na mabao manane na asisti saba, Elie Mpanzu (mabao saba, asisti 10) na Libasse Gueye (mabao saba), katika kuzalisha mabao mengi kwenye michuano mbalimbali.

Endapo Simba na Selemani Mwalimu, aliyemaliza msimu uliopita akiwa na mabao tisa, hawatamalizana kutokana na klabu inayommiliki, Wydad, basi Dala anaweza kuwa nyongeza muhimu katika eneo la ushambuliaji.

“Dala yupo na Simba kambini. Kama kila kitu kitakuwa kimekamilika, basi kuna uwezekano mkubwa akafanywa kuwa sapraizi katika utambulisho wa wachezaji kwenye tamasha la Simba Day,” kilisema chanzo hicho.

DALAS02

DALA NI NANI?

Staa huyo alizaliwa Julai 13, 1996, mjini Luanda, Angola, na kwa sasa ana umri wa miaka 30. Ana urefu wa mita 1.75 (futi 5 na inchi 9).

Timu yake ya mwisho kuichezea ilikuwa Al-Wakrah ya Qatar, klabu iliyoanzishwa mwaka 1959.

Katika maisha yake ya soka, Dala amewahi kuzichezea klabu za 1º de Agosto, Sporting B, Sporting CP, Rio Ave kwa mkopo, Antalyaspor kwa mkopo, kabla ya kurejea Rio Ave na baadaye kujiunga na Al-Wakrah.


KANTE NJIANI?

Endapo Dala atamalizana na Simba, kuna taarifa za ndani kwamba huenda klabu hiyo ikafanya mabadiliko katika eneo la kiungo mkabaji, ikiwamo uwezekano wa kumuuza Alassane Kante.

Katika nafasi hiyo, Simba tayari ina Kelvin Nashon, ingizo jipya kutoka Pamba, pamoja na Yusuph Kagoma.

Hivyo, macho ya mashabiki wa Simba yataelekezwa zaidi kwenye sehemu ya utambulisho wa kikosi leo, ambako huenda klabu hiyo ikawaandalia sapraizi kubwa.