Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Salum Akida aiokoa Polisi

TAKUKURU Pict

Muktasari:

  • Tanzania ni miongoni mwa nchi tatu za Afrika Mashariki, pamoja na Kenya na Uganda, zitakazokuwa wenyeji wa mashindano ya AFCON 2027

MABAO mawili yaliyofungwa na straika wa Polisi, Salum Akida ‘Bauno’ yameiokoa na kipigo kutoka kwa KMKM katika mchezo wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) uliochezwa kwenye Uwanja wa Mao A, Unguja.

Mshambuliaji huyo alifunga mabao hayo na kuisawazishia Polisi baada ya KMKM kuongoza 2-0 yaliyofungwa na Mateo Anton dakika ya 45 na 66 kwa mkwaju wa penalti.

Hadi dakika ya 66, Polisi SC ilikuwa nyuma kwa mabao 2-0, hali iliyowafanya baadhi ya mashabiki wa soka waliojitokeza kushuhudia mchezo huo kuamini kuwa KMKM ingeondoka na ushindi.

Mambo yalibadilika baada ya Polisi kuanza kufanya mashambulizi mfululizo na haraka kwenye lango la KMKM ambapo yalizaa matunda dakika ya 71 kwa straika huyo kufunga bao na kurudisha matumaini.

Akida ameongeza presha kwa KMKM, dakika ya 83 akafunga la pili na kuifanya Polisi SC kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya KMKM.

Matokeo hayo yameifanya Polisi SC kubaki nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 22.