Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namba mpya zaipa Arsenal ubingwa EPL

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Matokeo hayo yanaifanya City kupoteza mechi tatu mfululizo, na kuwa timu ya pili pekee katika historia ya Ligi Kuu England, baada ya Sheffield Wednesday msimu wa 1904-05, kushinda mechi zake saba za kwanza za msimu na kisha kupoteza tatu zilizofuata.

LONDON, ENGLAND: MECHI za raundi ya 10 za Ligi Kuu England zilitoka na jipya; Arsenal kwa sasa ndio mabingwa watarajiwa wa Ligi Kuu England, wakipewa zaidi ya asilimia 70 kutetea ndoo waliyotwaa msimu uliopita.

Kipigo cha mabao 3-1 ilichokipata Manchester City kutoka kwa Nottingham Forest ugenini kimeibua utabiri mpya unaouelekeza ubingwa wa ligi hiyo inayofuatiliwa zaidi duniani mikononi mwa Arsenal ambao wamepoteza mechi moja tu msimu huu ilhali wapinzani wao hao wakipoteza tatu wakiwa pia katika nafasi ya tatu.

Matokeo hayo yanaifanya City kupoteza mechi tatu mfululizo, na kuwa timu ya pili pekee katika historia ya Ligi Kuu England, baada ya Sheffield Wednesday msimu wa 1904-05, kushinda mechi zake saba za kwanza za msimu na kisha kupoteza tatu zilizofuata.

Arsenal, kwa upande mwingine, haikuvuruga baada ya matokeo yao pekee mabaya ya msimu kwani walijibu kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Brighton mwezi Septemba kwa kushinda mechi tano mfululizo za Ligi Kuu England.

ARSEN 01

Na sasa wameshinda mechi tisa kati ya 10 walizocheza 2026-27, na katika mchakato huo wamefikia idadi yao bora zaidi ya pointi baada ya mechi 10, pointi 27, sawa na msimu wa 2022-23.

Ikiijumuisha Arsenal ya misimu minne iliyopita, kuna mifano sita pekee ya timu iliyokusanya angalau pointi 27 katika mechi 10 za kwanza za msimu wa Ligi Kuu England. Timu nne kati ya hizo ziliendelea hadi kutwaa ubingwa, huku nyingine mbili zikimaliza nafasi ya pili.

ARSEN 02

Hata hivyo, timu mbili zilizomaliza nafasi ya pili zilikuwa Newcastle United 1995-96, iliyosambaratika maarufu huku Manchester United ikiifuatilia kwa karibu, na Arsenal ya 2022-23, ambayo ilikuwa timu tofauti kabisa na hii ya sasa.

Ni wachache wanaotarajia Arsenal kupoteza mwelekeo safari hii, na huenda hata kusiwe na mpinzani anayesubiri kutumia nafasi ya wao kuteleza.

Kwa mujibu wa Opta, Arsenal ilikuwa na nafasi ya asilimia 71.3 ya kutwaa ubingwa kabla ya mchezo uliopita kuanza, na hiyo iliongezeka hadi asilimia 71.9 baada ya ushindi dhidi ya Hull.

Lakini matokeo ya City yalikuwa na athari kubwa zaidi. Baada ya kipigo, nafasi za Arsenal kutwaa ubingwa zilipanda hadi asilimia 74.9 ilhali City sasa inapewa asilimia 14.3 urejea na kutwaa ubingwa.

ARSEN 03

Bila shaka, kuna timu nyingine zinazoshika nafasi za juu, na Brighton inayofanya vizuri haipaswi kupuuzwa. Hata hivyo, nafasi yake ya ubingwa ya asilimia 6.2 inaonyesha kuwa ni timu inayochukuliwa kuwa ya nje ya mbio.

Uwezekano wa Brighton kuendelea na kasi yake ya sasa kileleni mwa msimamo huku ikishiriki pia Europa League ni jambo moja; lakini pia inahitaji Arsenal kuanza kupoteza pointi kwa kiwango kikubwa zaidi.

Hata hivyo, Arsenal ikiwa imara kiasi hiki katika ulinzi, inaonekana hakuna timu inayoweza kuifikia. Wana ulinzi bora zaidi katika Ligi Kuu England msimu huu wakiwa wamefungwa mabao matano katika mechi 10, na pia wamewaruhusu wapinzani wao kupata kiwango cha chini zaidi cha mabao yanayotarajiwa kufungwa (7.6), kwa tofauti kubwa. Ubingwa wa Ligi Kuu England sasa uko mikononi mwa Arsenal kuupoteza.