Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Safu ya ulinzi tatizo JKU

JKU Pict

Kocha Mkuu wa JKU, AbdulSaleh Mohammed amefichua udhaifu mkubwa unaoendelea kuitafuna timu hiyo akisisitiza kuwa safu ya ulinzi bado ni tatizo sugu linalohitaji ufumbuzi wa haraka.

Akizungumza Mwanaspoti, kocha huyo amesema haridhishwi na ngome yake ya ulinzi inavyoruhusu mabao kwa urahisi katika michezo ya Ligi Kuu Zanzibar.

“Mabeki wamekuwa wakipoteza umakini katika dakika za mchezo, jambo ambalo linaigharimu timu na kuondoa taswira halisi ya ushindani wa kikosi hicho,” amesema.

Amesema, licha ya safu ya ushambuliaji kupambana na kufunga mabao katika kila mchezo, kocha huyo alieleza kuwa juhudi hizo zinapotezwa bure kutokana na urahisi wa safu hiyo kuruhusu nyavu zao kutikiswa.

Amesema uwiano mbaya kati ya kufunga na kuruhusu mabao ni changamoto kubwa inayotishia malengo yao ya msimu huu.

Alisisitiza kuwa timu inajipanga kufanya mabadiliko ya kifikra na kiufundi kwa wachezaji wa eneo la nyuma.

Ameongeza kuwa nidhamu ya ukabaji na mawasiliano thabiti kati ya kipa na mabeki wa kati ni maeneo ya kwanza wanayoyapa wanaendelea kuyapata kipaumbele kwenye uwanja wa mazoezi.