Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rayon Sports yaifuata Gor Mahia fainali Kagame

RAYON Pict

Muktasari:

  • Ushindi huo umeifanya Rayon kuendeleza rekodi yake ya ushindi wa asilimia 100 tangu kuanza kwa mashindano hayo ambapo sasa ina kibarua cha kuvaana na Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa fainali utakaopigwa Agosti 7, 2026 kwenye Uwanja wa Amahoro.

MIAMBA ya soka la Rwanda, Rayon Sports, imetinga fainali ya Kombe la CECAFA Kagame 2026 baada ya kuichapa Jamus SC ya Sudan Kusini mabao 3-1 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Kigali Pele.

Ushindi huo umeifanya Rayon kuendeleza rekodi yake ya ushindi wa asilimia 100 tangu kuanza kwa mashindano hayo ambapo sasa ina kibarua cha kuvaana na Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa fainali utakaopigwa Agosti 7, 2026 kwenye Uwanja wa Amahoro.

Rayon iliyomaliza kinara wa Kundi C kwa kushinda mechi zote tatu za hatua ya makundi, ilianza kuonyesha ubora wake mapema baada ya kiungo wa kimataifa wa Burundi, Akbar Muderi kuifungia bao la kwanza dakika ya 17.

RAYO 01

Baada ya kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0, Rayon ilirejea kipindi cha pili ikiwa na kasi ileile na kuongeza bao la pili kupitia Ibrahim Djingarey dakika ya 57, hatua iliyowapa utulivu mashabiki wao waliojitokeza kwa wingi.

Jamus ambayo imekuwa moja ya timu zilizoshangaza wengi kwenye mashindano haya, ilirejea mchezoni dakika ya 70 baada ya Bandjouhou kufunga bao la kupunguza tofauti na kufufua matumaini ya kusawazisha.

RAYO 02

Hata hivyo, wakati Jamus ikipambana kusaka bao la pili, ilijikuta ikiacha mianya ambayo Rayon Sports ikaitumia na kupata bao la tatu lililofungwa na Gloire Tambwe dakika ya 86 na kuzima kabisa ndoto za wawakilishi hao wa Sudan Kusini.

Ushindi huo uliwafanya maelfu ya mashabiki wa Rayon Sports kuondoka Uwanja wa Kigali Pele wakishangilia, wakiamini timu yao ipo hatua moja tu kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Kwa matokeo hayo, fainali ya mwaka huu itawakutanisha Rayon Sports na Gor Mahia  huku Jamus SC ikitarajiwa kucheza mchezo wa kusaka nafasi ya tatu dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

RAYO 03

Mbali na heshima ya kutwaa ubingwa wa CECAFA Kagame, timu zitakazomaliza katika nafasi za juu pia zitajinyakulia zawadi nono za fedha. 

Bingwa ataondoka na dola  30,000 (Sh79.3 milioni), nafasi ya pili atapata dola 20,000 (Sh52.9 milioni) huku wa tatu akiondoka na dola 10,000 (Sh26.4 milioni).